Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wametoa maoni yao kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika nyanja tofauti ikiwemo utawala bora, uchumi, amani, utulivu na umoja katika kongamano la maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Kongamano hilo ambalo limefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mh. Janeth Mayanja ambaye aliongoza mdahalo kwa kupata maoni ya wadau mbalimbali pamoja na wananchi katika maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo kuelekea 2050.
Akizungumza wakati akifungua Kongamano hilo DC Janeth Mayanja amesema kuwa ili kufikia malengo ya dira 2050, serikali imeweka jitihada ya kuandaa dira mpya ya maendeleo ya taifa ambayo itakwenda mpaka 2050 kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali pamoja na wananchi kuchukua maoni yao wanapendekeza nini katika Tanzania waitakayo kufikia 2050.
Amesema kuwa maoni ya wananchi ni muhimu sana katika maandalizi ya dira hiyo na kusisitiza kuwa serikali itafanyia kazi maoni yote ya wananchi ili kuwa na mpango wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025-2050 ulioshirikisha wananchi wote.
Aidha, amewataka wadau wa maendeleo na wananchi kujikita katika kutoa maoni yenye manufaa kuhusu muelekeo wa maendeleo wanayotaka kufukia ifikapo 2050.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.