Idara ya Afya ni miongoni mwa Idara 13 zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Idara hii ina jumla ya vituo vya kutolea huduma vipatavyo 63 ambapo Hospitali ya Wilaya ni 1, Vituo vya Afya ni 5, na Zahanati 57.
Vile vile, Idara ya Afya inatoa huduma kwa jamii kama ifuatavyo:-
1. Huduma ya wagonjwa wa nje yaani (OPD),
2. Huduma ya kulaza wagonjwa yaani (Inpatient),
3. Huduma ya upasuaji mkubwa na mdogo,
4. Huduma ya mama na mtoto yaani (RCH),
5. Huduma ya CTC,
6. Huduma ya Kifua Kikuu na Ukoma,
7. Huduma ya wazee, huduma ya wagonjwa wa akili,
8. Huduma ya kinywa na meno, na
9. Huduma ya kuwasubirisha wamama wajawazito wenye vidokezo hatarishi (CHIGONELA).
Aidha, kuna Jengo la grade “A” kwa ajili ya kulaza wagonjwa wa makundi maalum, mfano bima ya afya na kadhalika.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.