Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Bi. Tulinagwe Ngonile (Afisa Elimu sekondari) leo Agosti 19, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, amezindua mafunzo ya siku tatu kwa kamati ya CAMFED (Campaign for Female Education) Wilaya ya Chamwino, ili kuijengea uwezo wa kiutendaji katika kutekeleza majukumu yake.
Kamati hiyo ina majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuratibu na kusimamia zoezi la upatikanaji wa wanafunzi wa sekondari wanaohitaji ufadhili wa masomo kutoka kaya maskini.
Idadi ya wanafunzi wanaonufaika na ufadhili wa shirika hilo kwa mwaka huu pekee ni 1,735 kwa kidato cha pili hadi cha sita, wanafunzi 24 katika vyuo vya ufundi, na wanafunzi 7 katika ngazi ya stashahada.
Shirika la CAMFED lilianza shughuli zake katika Wilaya ya Chamwino mwaka 2021, ikiwa ni wilaya pekee ya mkoa wa Dodoma inayonufaika na miradi ya shirika hilo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.