Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki amewataka watanzania kutong'angania Kuwa na Idadi Kubwa ya Mifugo,badala yake amewataka kuwa na na Mifugo inayoendana na Malisho ili kukidhi mahitaji ya mifugo.
Mhe. Mashimba Ndaki, ameyasema hayo wakati wa sherehe za ufunguzi wa Nanenane kanda ya kati yaliyofanyika Augosti 5, 2022 ambayo yalihusisha mikoa ya Dodoma na Singida.
Akizungumza katika maonesho hayo Mhe. Mashimba alisema kuwa Maonesho ya Nanenane yanalenga katika kujitangaza pamoja na kutoa elimu huku akibainisha kuwa Mwaka huu maonesho ya nanenane mkoa wa Dodoma ni maonesho ya 14 na paredi ya 11.
"Paredi hii imehusiha watu wachache hivyo ni matumaini yangu kuwa Paredi ya mwaka kesho (2023) itajumuisha watu wengi zaidi,Hongereni sana kwa ubunifu huu mzuri,Taarifa yetu ya uchumi , inaonyesha ukuaji wa kilimo umepungua kufikia 3.39% (2021) toka 4.99%(2020) ikionyesha kwamba uchumi umepungua kwa 1%. Sababu za upungufu huo ni pamoja na ukame/ ukosefu wa mvua pamoja na Uviko-19. Hata hivyo Serikali imepanga tutoke kwenye kilimo cha kujikimu na kuhamia katika kilimo cha kibiashara, kilimo chetu kinakabiliwa na Changamoto ya tabia nchi, kwa kuliona hilo serikali imeongeza bajeti za kilimo, mwaka huu zimetengewa fedha za kutosha na hivyo kusaidia kukabiliana na Changamoto hizo" Alisema hayo Mhe.Mashimba Ndaki
Sanjari na hayo Mhe. Ndaki aliziagiza taasisi zinazofanya tafiti za kilimo,kufanya tafiti ambazo zitasaidia wananchi kwani kufanya hivyo watakua wamegusa maisha ya wananchi huku akieleza kuwa kwa sasa bei za bidhaa Kwa wananchi zipo juu sana.
"Ili bidhaa hizo ziweze kuwafikia watanzania basi ni bora bei ziendane na kipato cha wananchi pamoja na ubora wa bidhaa zetu ni lazima tuangalie jinsi ambavyo tunapakia/tunafunga bidhaa zetu, kwani tunatakiwa kushindanisha ubora ambao ni pamoja na jinsi bidhaa ilivyofungwa"Mhe.Masimba Ndaki
Aidha Mhe. Ndaki alitumia nafasi hiyo kumpongeza mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwa kuaminiwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na kuhamishiwa makao Makuu ya nchi. “Dodoma ni makao makuu ya nchi, hivyo kwa kuhamishiwa Dodoma inaonyesha kwamba Mhe. Rais ana imani na wewe kwamba utamsaidia “. Alisema Mhe. Ndaki.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alieleza kuwa Mkoa wa Dodoma una idadi ya mifugo milioni 5.64 ambapo kati ya mifugo hiyo ng’ombe wa kienyeji ni millioni 1.53 na 242,000 ni ngombe wa kisasa.
Alisema kuwa Mkoa wa Dodoma una eneo la ufugaji wa samaki," tunayo teknolojia ambayo itatupelekea kufuga samaki kwa njia ya kisasa,rai yangu sisi hapa Dodoma tutajitahidi sana kuona kwamba tunafuga na kujitosheleza kwa samaki"Rosemary Senyamule mkuu wa mkoa Dodoma.
Aidha mhe.Senyamule alisema kuwa Kwa upande wa kilimo mwaka huu mkoa wa Dodoma unatarajia kuvuna kwa 55% ,Dodoma imeanishwa kama mkoa mmoja wapo kati ya mikoa mitano ambayo inafaa kwa kulima alizeti,hivyo kazi kubwa, ni kuhakikisha kuwa tunafanya kazi kwa bidii na kuifanya Dodoma kuwa ya mfano.
"Nitumie fursa hii kuwakumbusha Mambo matatu, kwanza Mkoa wa Dodoma ni mkoa mmojawapo wenye ukubwa wa vyuo vikuu hivyo tunataka tuone matokeo ya vyuo vikuu Dodoma kwa wananchi wa Dodoma. Jambo la pili Machinjio yamelegalega kwa hiyo itabidi tukutane na tuongee namna tunavyoweza kuyaboresha.Tatu, 16/8/2022, Wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenye maeneo yote ambayo Mwenge utapita.Pia kutakuwa na Sensa ya watu na Makazi 23/8/2022 ".amesema Mhe. Senyamule.
Aidha Mhe.Senyamule alimweleza Mhe.Waziri Mashimba Ndaki kuwa , uwanja wa nanenane Nzuguni ni uwanja mkubwa sana hivyo nitaomba tukutane ili tuone namna bora ya kuboresha huu uwanja na ili uonekane kuwa ni wa makao makuu.
Kaimu Katibu Mkuu, Dkt.Charles Mhina ambaye amemwakilisha Bw.Tickson Nzunda Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi – Sekta ya Mifugo ameeleza kuwa Wizara inaendelea kuboresha na kuzalisha mbegu kupitia vituo vyao mbalimbali na inajipanga kutoka kwenye ufugaji usio na tija hadi ufugaji wenye tija. Aidha ameahidi kuwa watandelea kuimalisha uzalishaji kwa kuwapatia wafugaji mbegu za malisho, ili wafugaji nao waweze kuzalisha kwa kutumia tija.
Nae Katibu Mkuu sekta ya Uvuvi. Rashid Tamatama . Alitoa shukrani kwa kamati ya maandalizi na wana Dodoma kwa maandalizi mazuri ya maonesho haya kwani yanatoa fursa wananchi kujua sekta ya mifugo na uvuvi.
Alisema kuwa Mwaka 2021 sekta ya uvuvi iliongeza Vizimba 731 ambavyo vililenga wafugaji wadogowadogo na kubainisha kuwa Serikali imedhamiria kupunguza mazao ya uvuvi na kuongeza thamani.
"Tumepanga kuongeza uzalishaji kimkakati kwa ujenzi wa bandali ya uvuvi Kilwa,tumeboresha huduma za ugani, hivyo endapo unataka kuanza ufugaji wa Samaki fika ofisini na wataalam watakuelimisha, Nawasihi wananchi wa Dodoma na Singida kuhudhuria kwa wingi ili kuweza kujifunza masuala ya mifugo na uvuvi’’.Amesema Tamatama.
Akizungumzia paredi ya Wanyama, Jeremia Temu kiongozi wa paredi ya mifugo,alieleza lengo la paredi hiyo ni kutoa elimu kwa wafugaji kuwa na ufugaji wenye tija unaowezekana na kuonyesha fursa za kibiashara kwamba wanaweza fanya ufugaji bora.Alisema kuwa Paredi hiyo itaonyesha ufugaji bora unawezekana na Ufugaji bora huanza na mbegu bora zilizothibitishwa. Paredi hiyo ilianza kwa kuonyesha ngombe wa maziwa, ngombe wa nyama na hatimae mbuzi. Ngombe mbalimbali walipita na kuonyesha manufaa yake. Ngombe waliopita ni pamoja na Ng’ombe wa maziwa Mama Tony ambaye anzalisha lita 22 za maziwa kwa siku, Gwasi lita 33 kwa siku,Morning light Lita 30 kwa siku, Mkombozi lita 28 kwa siku, Mathayo lita 16 kwa siku.
Aidha pamoja na ng’ombe wa maziwa Ngombe wa Nyama nao walipitishwa kwenye paredi hilo ambapo ng’ombe Mahinyila ana 579kg,Masanja 590kgs na Kikwete700kgs.
Akimalizia Mratibu wa Nanenane Bi. Aziza Mumba ameeleza kuwa haya ni maoenesho ya 14 na paredi ya 11, ambapo kutakuwa na mashindano ya wanyama kwa wafugaji wakubwa na wafugaji wadogo.Kutakuwa na Makundi manne ya ushindani.Lengo letu la hapo baadae ni kuufanya uwanja wa Nanenane Nzuguni kuwa uwanja wa viwango vya kimataifa.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.