Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mheshimiwa Vumilia Nyamoga ameipongeza Idara ya Elimu Sekondari kwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne 2020 na kuifanya Wilaya kuwa ya kwanza kimkoa ambapo kwa mwaka huu ufaulu umepanda hadi kufikia asilimia 92.1
Ametoa pongezi hizo jana tarehe 28 Januari 2021 wakati akitoa salamu zake kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya pili ya mwaka wa bajeti 2020/2021 kilichofanyika kaitika ukumbi wa serikali ya kijiji cha Chamwino.
‘Nipende kuwapongeza Idara ya Elimu Sekondari kwakututoa kimasomaso kwa Wilaya yetu ya Chamwino kushika nafasi ya kwanza Mkoa wa Dodoma, hakika Afisa Elimu Sekondari na timu yako mmefanyakazi nzuri kuinua kiwango cha ufaulu kwa Wilaya yetu ya Chamwino” amesema Mh. Nyamoga
Mh. Nyamoga amesema kuwa kwa sasa Wilaya hii inaangaliwa kwa jicho la tatu ikizingatiwa kuwa ndio Wilaya ambapo tunakaa na Mheshimiwa Rais wetu hivyo tusimuangushe katika kutekeleza majukumu yetu.
Pia ametumia fursa hiyo kuwashukuru Waheshimiwa Madiwani kwa ushirikiano wanaompatia hasa katika suala zima la kuhimiza ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya kidato cha kwanza katika kata zao , amewahimiza waheshimiwa kumalizia kwa wale ambao bado ili ikiwezekana hadi kufiakia tarehe 28 Februari, 2021 wanafunzi wote waliokosa nafasi kwa kipindi cha kwanza wawewamesharipoti shuleni na kuanza masomo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.