Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga ameagiza viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha wametoa elimu kwa watumishi wa Umma na wananchi kwa jumla kuhusu uwepo wa kituo cha kutolea huduma kwa wateja kilichoanzishwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Akiongea kwenye ziara iliyofanywa na waandishi wa habari katika kituo hicho Mhandisi Mnyamhanga amesema lengo lakuanzishwa Kwake nikuwaondolea adha watumishi wa Umma na wananchi kwa ujumla kusafiri mpaka makao makuu Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ajili ya kupata huduma.
Amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI inahudumia wateja mbalimbali ikizingatiwa kuwa ndio Wasimamizi wa mikoa 26, Wilaya 139, Halmashauri 185, Tarafa 570, Kata 3956, Vijiji 12319, Mitaa 4263, Vitongoji 12384 na zaidi ya watumishi asilimia 73 wanatoka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hivyo ni vema kituo cha kutolea huduma kwa wateja kilichoanzishwa kikatangazwa kuanzia ngazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Amefafanua Kuwa kujulikana kwa kituo hicho kitasaidia kupunguza mlundikano wa watumishi wa Umma na wananchi kwa ujumla kwenda katika Ofisi ya Makao makuu kupata huduma.
Ametoa wito kwa wananchi wote wanaohitaji kupata huduma mbalimbali katika Ofisi ya Rais TAMISEMI kukitumia kituo hicho ilikuweza kupata huduma stahiki kwa haraka na amewaagiza watumishi wote kuhakikisha wanakitangaza ili wananchi wakijue na kukitumia.
Akitoa taarifa ya mafanikio msimamizi wa kituo Bi. Antelma Mtemalanji amesema mpaka sasa wameweza kupokea simu 15,886 ambapo wateja waliosajiliwa ni 5571 na hoja zilizokamilika na kufungwa ni 5571.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.