Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Isaya Msuya amewataka madereva bodaboda kufuata sheria, taratibu na kanuni zinazowaongoza katika kazi yao na kwa kufanya hivyo wataweza kusaidiwa mikopo kwa ajili ya kununua pikipki zao wenyewe kupitia vikundi watakavyoviunda.
Ahadi hiyo ameitoa alipokuwa kwenye hafla ya kukabidhi vyeti kwa mabodaboda 171 waliohitimu mafunzo ya udereva wa pikipiki Novemba 24, 2023 ambapo alikuwa mgeni rasmi. Mafunzo yaliyotolewa na chuo cha Wide Driving Institute cha mkoani Dodoma.
Ameahidi pia kutoa leseni kwa madereva bodaboda waliohitimu mfunzo isipokuwa ameeleza kuwa wanachopaswa kufanya ni kuwa na TIN namba , namba ya NIDA pamoja na kulipia gharama za leseni, na amesema atatoa maelekezo kwa maafisa wa NIDA na TRA kutoa ushirikiano unaohitajika ili waweze kupata vitu hivyo kwa urahisi
" Ofisi ya Mkuu wa wilaya itahakikisha inawezesha upatikanaji wa leseni kwa urahisi, ofisi ya NIDA iko chini ya Mkuu wa Wilaya, lakini pia Ofisi ya TRA iko chini ya Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Wilaya ndio mwenyekiti wa kamati ya mapato ya Wilaya kwa hiyo hayo mengine ni maelekezo tu." Alisema Mkuu wa Wilaya.
Aidha amewashukuru chuo cha Wide Driving Institute kwa kukubali ombi la Serikali la kutoa mafunzo kwa bodaboda hao.
"Natoa pongezi kwa viongozi mbalimbali nikianza na chuo cha Wide Driving Intitute, baada ya Serikali kuzungumza na ninyi kuwaomba kwamba tuna clash program ya kuwanoa vijana wetu maafisa usafirishaji, tunahitaji wapatiwe elimu ya kuendesha vyombo vya moto, lakini namnaya kuzuia ajali nyigi ambazo zinatokea, waweze kupata mafunzo hayo. Hamkusita bali mlikubali kwa moyo mmoja." Alisema Mkuu wa Wilaya.
"Na gharama ilikuwa ni kubwa sana toka 75, 000/= wao walikubali kutoa kwa gharama ya 20,000/= kwa hiyo wametusaidia kwa kiasi kikubwa hii ni kazi nzuri iliyofanywa na Wide Driving Institute. Japo najua gharama hizi mmelipia wenyewe lakini najua nisehemu ya uwajibikaji maana mkilipiwa kila kitu baada ya kwenda kusoma hata ulichojifunza utaona hakina maana." Alisema Mkuu wa Wilaya.
Aliishukuru pia Ofisi ya Polisi Wilaya kupitia Mkuu wa usalama barabarani Wilaya kwa kuhakikisha mambo yote yanawezekana, ofisi ya Mkurugenzi kwa kushiriki kikamilifu kuhakikisha haya yanayofanyika leo yaweze kutokea, alimshukuru pia Mhe. Mbunge wa jimbo la Chamwino walipomfikishia wazo hili, angekuwa ni kiongozi asiyefahamu jambo hili angeweza kulipinga, lakini alikubali nakuunga mkono kwa asilimia mia moja wakishirikiana na Mhe. Diwani wa Buigiri.
Aliendelea kueleza kuwa mbunge aliahidi kuwajengea bodaboda vibanda kwa ajili ya kujikinga jua na mvua. Aliwashukuru pia LATRA.
Mkuu wa Wilaya alielekeza bodaboda kujisajili ofisi ya mkurugenzi na kuunda vituo ili wawe rasmi.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.