Wazazi Chamwino Waaswa kutimiza Wajibu kwa Haki za Watoto
Wazazi na wadau wanaohusika na malezi ya watoto Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wametakiwa kutimiza wajibu wao katika kutekekeleza haki za watoto. Hayo yamesemwa na Ndugu Sixfrid Paul Yamay Afisa Tarafa Mvumi, ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Wilaya ya Chamwino Bi Neema Nyalege ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika leo, tarehe 16, Juni 2022 katika shule ya Sekondari DCT iliyopo Kata ya Mvumi mision."Naomba Watotonisisitize kwamba wazazi na wadau wote wanaohusika na malezi ya watoto wanajibika kuhakikisha kwamba mtoto anapata haki yake". Alisema Yamay.Amewataka pia wazazi kuhakikisha wanawalea watoto katika malezi bora yatayowaandaa watoto kuishi maisha bora ya baadae.Mgeni Rasmi amewaelekeza watoto kuishi katika ndoto zao, kama mtoto anandoto ya kuwa mtu fulani anao wajibu wa kuishi ndoto hiyo.Aidha wazazi wameaswa pia kuwapatia malezi bora watoto yatakayowalinda dhidi ya ukatili ikiwa ni pamoja na kuwapatia lishe bora kutoka kweye makundi matano ya chakula yatakayowawezesha kukua katika afya bora.Katika maadhimisho hayo Halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo SAT, Wafanyakazi wa Kata ya Mvumi Mision, Compassion wametoa vifaa vya shule pamoja na sabuni za kufulia.Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni " Tuimarishe ulinzi wa mtoto,Tokomeza ukatili dhidi yake."
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.