Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imezidi kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani katika kipindi cha miaka 3 kutokana na jitihada za Menejiment ya Halmashauri chini ya usimamizi wa Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Athumani Masasi.
Mwaka 2016/2017 ilikusanya shilingi bilioni 1.205 sawa na 76% ya lengo la makusanyo.
Mwaka 2017/2018 ilikusanya shilingi bilioni 1.481 sawa na 93%.
Mwaka 2018/2019 imekusanya shilingi bilioni 1.742 sawa na asilimia 113% ya lengo la makusanyo.
Aidha katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imeweka mikakati madhubuti na imelenga kukusanya shilingi bilioni 2.4
Vyanzo vikuu vya mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ni ushuru wa Mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Leseni za Biashara.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.