Asema Wananchi Wajiunge na CHF Hospitali Dawa Zipo za Kutosha
Kauli hiyo imetolewa Julai 24, 2019 na Katibu Tawala wa Wilaya ya Chamwino Bi. Juliana Kilasara alipokuwa kwenye ziara ya uhamasishaji wa wananchi kujiunga na CHF iliyoboreshwa katika kata ya Mvumi Mission.
Bi. Kilasara amezungumza na viongozi na watendaji wa kata na kuwataka kuwahamasisha wananchi kujiunga na CHF.
Katika kikao hicho Mwenyekiti wa Kijiji cha Chihembe Bwana Yoram Matonya alieleza hofu ya wananchi ya kutopata dawa na huduma nzuri wanapoenda kutibiwa wakiwa na kadi za CHF.
Hali hii ilimlazimu Katibu Tawala kuhamishia kikao katika Hospitali Teule ya Wilaya iliyopo kwenye kata ya hiyo ili kujiridhisha na kiwango cha dawa kilichopo.
Akiwa hospitalini hapo Katibu Tawala huyo ametembelea chumba cha kuhifadhia dawa na maeneo mengine ya kutolea huduma ili kujiridhisha.
Nae Mganga Mkuu Dkt. Asteria Mpoto ameeleza kuwa Serikali inapeleka dawa na vifaa tiba kwa vituo vyote vya matibabu na katika Wilaya ya Chamwino hali ya utoaji wa huduma za afya umeimarika.
"Nimejionea hali halisi, nendeni muwaeleze wananchi wajiandikishe CHF dawa na vifaa tiba vipo vya kutosha" alimalizia Katibu Tawala.
Bwana Abel Angelbert Mfamasia wa Wilaya (kushoto) akitoa maelezo ya hali ya dawa kwenye Hospitali Teule ya Mvumi
Mratibu wa CHF Wilaya ya Chamwino Bw. Dennis Vagela akizungumza na viongozi wa kata na vijiji, watendaji, wataalam na wadau wa afya kata ya Mvumi Mission kabla ya kwenda Hospitali ya Wilaya
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.