Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kupitia mdau wake taasis ya LEAD Foundation inayoendesha mradi wa Kisiki Hai imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza kwenye shindano lililohusu masuala ya kilimo hifadhi makinga maji na utunzaji wa vyanzo vya maji, utungaji wa nyimbo za mazingira, mchezo wa mpira wa miguu na mpira wa pete.
Mshindi wa kwanza alikabidhiwa ngao na ngao hiyo imekabidhiwa kwa Mkurugenzi Mtendaji na Bi Happy Mkalawa mratibu wa mradi wa Kisiki hai Chamwino leo Novemba 3, 2023 na kupokelewa kwa niaba ya Mkurugenzi na Bibi Prudence Kaaya Ching'ole Ofisini kwake.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo mratibu mradi wa Kisiki Hai ameeleza kuwa zipo hatua nne za kutunza kisiki hai ya kwanza ni kuchagua au kukitambua kisiki hai.
" unaangalia matawi ambayo yameshiba na yanakuwa kuelekea juu, ambayo hayana afya yanapaswa kuondolewa ili kupunguza ushindani wa chakula nà hewa." Alisema Mkalawa.
Alieleza hatua ya pili ni kupogolea ambayo ni hatua ya kuondoa matawi yasiyohitajika. Aliendelea kueleza kuwa unapopogolea unapaswa kuangalia kifaa kiwe na makali ya kutosha, makali yaelekee juu yasielekee chini ilikusudi usijeruhi mti. Mti ukipata jeraha inakuwa rahisi kukaribisha wadudu wakaushambulia.
Vilevile alieleza kuwa haipaswi kupogolea karibu na maungio angalau utoke nje kidogo ya maungi ya tawi la mti.
Mratibu alieleza pia kuwa hatua ya tatu ni kuweka alama kujulisha kuwa mti ni wa kisiki hai hivyo unatunzwa na unatambulika.
" Unapaswa kufungwa kitambaa chenye rangi yeyote ile ambayo inaweza ikatambulisha jamii kwa namna yeyote ile kuwa hiki ni kisiki hai na kinatunzwa." Alisema Mkalawa.
Hatua ya mwisho ilielezwa kuwa ni kutunza hivyo inashauliwa kuutembelea mara kwa mara ili kuona iwapo umeshambuliwa na wadudu au umevamiwa na mifugo lakini pia kama umexhipua zaidi ili uweze kuupogolea tena. Pia inashauliwa kuwa aawe amepanda mazao mengine kwenye shamba yatakayojfanya afike mara kwa mara kuangalia maendeleo ya visiki hai. Klielezwa kuwa anaweza kuwa amepanda mihogo au mbaazi.
Wilaya zilizoshiriki kwenye mashindano haya ni Chamwino kutoka mkoa wa Dodoma na Ikungi kutoka mkoa wa Singida.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.