Wilaya ya Chamwino imenufaika na fedha za miradi ya maendeleo takribani shilingi bilioni 57.8 zilizotolewa na Serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali katika sekta za elimu, afya, kilimo na ardhi.
Haya yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Dkt. Semistatus H. Mashimba leo Novemba mosi, 2023 kwenye ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Dodoma wakati wa tukio la uzinduzi wa kampeni ya TUMEKUSIKIA NA TUMEKUFIKIA ambayo inalenga kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita.
Kwa upande wa elimu Chamwino imepata shilingi bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya wasichana ya mkoa itakayohudumia wanafunzi wasichana wa mkoa wa Dodoma na mikoa jirani.
" Tumepata shilingi bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa shule moja ya sekondari ya wasichana ya mkoa ambayo itahudumia waschana wetu wa mkoa wa Dodoma na mikoa jirani."
Vilevile kata mbili za Handali na Haneti zilizokuwa na msongamano mkubwa wa wanafunzi ambapo imejengwa shule moja ya Mjeloo kwa shilingi milioni
" Tuna kata mbili zenye msongamano sana wa wanafunzi karibu watu elfu thelasini kwenye kata na hivyo kuwa na msongamano sana hususani shule za skondari, kunashule moja inaitwa handali ilikuwa inapokea takribani wqnafunzi 1817 na tumepokea fedha takribani milioni 811 kujenga shule mbili, moja inaitwa mjeloo ambapo katika shule hii imetoka kwenye wanafunzi 1817 na kuchukua wanafunzi 664."
" lakini kupitia shule nyingine ya Kwahemu Mhe Rais ameleta fedha. Ilikuwa inapokea wanafunzi 714, ikawa na msongamano mkubwa lkini kwa sasa tumejenga shule nyingine ya sekondari inaitwa Yobo imeshasajiliwa na inachukua wanafunzi 206 tumepunguza pia msongamano."
Aliendelea kueleza kuwa kwenye Idara ya elimu pia yamejengwa madarasa 64 ya UVIKO na madarasa 94 ya sekondari na maabara 6 na mradiwa BOOST umejenga madarasa 56.
" Kwa ujumla kwenye sekta hii ya elimu zimetolewa takribani bilioni 13.8 kwa ajili ya miundombinu ya Elimu."
Kwa upande wa Afya Mkurugenzi alieleza kuwa vimejengwa vituo vya Afya Vitatu vya Itiso, Manda na dabalo ambapo vituo hivi vyote vipya tumeongeza huduma muhimu kwa wqnanchi wetu ambazo ningependa niziseme. Ya kwanza tumeongeza huduma kwa watoto na mama wajawazito, lakini pia tumeongeza huduma za upasuaji, wananchi walikuwa wanatembea takribani kilometa120 kuja kupata hizo huduma. Lakini tumeleta vifaa vya tiba vya kisasa kabisa vya maabara na huduma zote za maabara zinzfanyika kwenye vituo vyetu.
Mhe. Rais amewasikia wananchi wa Chamwino na Kwenye vituo vya Afya tunakwenda kununua vyombo vya usafiri ambapo tumeanza na kituo cha Afya cha Handari, tumenunua ambulance mpya ambayo itahudumia wananchi takribani elfu 18.
Vilevile Mkurugenzi alieleza kuwa kuna mambo mengine muhimu ambayo yamefanyika kwenye Halmashauri, kuna vifaa muhimu kama XRay mashine, Utrasound ambavyo vimenunuliwa kwenye vituo vyetu vyote vya kutolea huduma takribani 37 lakini kubwa ni kwamba tulikuwa tunatoa huduma za upasuaji kwa vituo viwili tu lkini kwa sasa utaona Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani tumefikisha vituo saba. Kwa vijijini haya ni mafanikio makubwa sana.
Mkurugenzi pia alieleza kwenye Idara ya kilimo Mhe. Rais amewekeza takribani shilingi bilioni 48 kwenye maeneo matatu ya Chinangali ambapo kuna ekari 1200, lakini pia kunaeneo la Membe lenye hekari zaidi ya 8000, lakini pia eneo la ndogowe.
"Kimsingi miradi hii inakwenda kutatua mambo mawili makubwa la kwanza ni kuhusu vijana na wanawake ambapo kuna hekari 1000 kwa ajili yà vijana na wanawake." Alisema Dkt. Mashimba.
"Suala la pili ni suala la lishe kwenye mashule yetu, watoto wetu, haya ni mafanikio makubwa sana ambayo yanakwenda kuleta mabadiliko kwenye wilaya yetu hasa ukizingatia zile R 4 za Mhe. Rais ambapo alisema zitaleta mageuzi makubwa lakini na ujenzi mpya kupitia miradi hii mikubwa na kuhakikisha tunakuwa na mapinduzi makubwa ya uchumi kwa maana ya lishe na maendeleo ya wanachi kwa ujumla." Alisema Mkurugenzi Mtendaji.
Kuhusu suala la ardhi Mkurugenzi Mtendaji alieleza kuwa wanakata kama 36 lakini kupitia mradi wa benki ya Dunia ambao pia unashirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na wizara ya Ardhi tayari wamepima kata 12 na vijiji 60 vimefikiwa na mradi huu. Ilielezwa kuwa suala hili ni la muhimu sana katika kupanga na kumilikisha maeneo .
"Shughuli hii inaongeza thamani kwenye maeneo yetu lakini pia inavutia wawekezaji kwenye wilaya yetu ya Chamwino. Lakini zaidi katika hili niseme tu hapo awali kiwango cha utoaji hati kwa wilaya ya chamwino kwa mwaka wa fedha kilikuwa takribani hati 50 hadi 60 lakini tangu awamu ya sita imeingia madarakani tumefikia kiwango cha kutoa hati 400 mpaka 800 kwa mwaka wa fedha. Kwa kweli takwimu hizi zinaonyesha Serikali ya awamu ya sita imewasikia wananchi na imewafikia." Alisema Dkt. Mashimba.
Kampeni ya ya TUMEKUSIKIA TUMEKUFIKIA imezinduliwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nauye na kufungwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Festo Ndugange.
Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Staki Senyamule, Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg. Mobhare Matinyi na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za mkoa wa Dodoma.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.