Wizara ya Maliasili na utalii kwa Kushirikiana na Halmashauri.ya Wilaya ya Chamwino wamefanya kikao cha kupitisha Mpango wa Kanda wa Usimamizi wa Rasilimali (RZMP) Julai3, 2023. Kikao kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Baada ya kupata maoni ya wadau na kupitisha Mpango wa Kanda wa Usimamizi wa Rasilimali utawezesha eneo hilo kutangazwa kuwa Jumuiya ya Hifadhi na kupewa Haki ya Matumizi ya Rasilimali na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.
Wizara ya Maliasili na utalii kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Chamwino inaendelea na utekelezaji wa mradi wa kupambana na ujangili na uthibiti biashara haramu ya nyara katika maeneo ya mfumo wa ikolojia wa Ruaha - Rungwa.
Vijiji vya Ndogowe na Mlazo wamefanikiwa kuanzisha Hifadhi ya wanyamapori Jamii - Wildlife Management Area- WMA inayopakana na maeneo ya Hifadhi hasa hifadhi ya wanyamapori MBOMIPA - IRINGA. Vijiji hivi ni katiya vijiji 10 vya Tarafa ya Mpwayungu vinavyokabiliana na changamoto wanyamapori wakali na waharibifu.
Akizungumza alipokuwa akifungua kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino Dkt. Semistatus H. Mashimba amipongeza Wizara ya Maliasili na utalii kwa kufanikiwa kuanzisha WMA pamoja na wananchi waliokubali kuanzisha. Alimuahidi Mkurugenzi kutoka wizara ya Maliasili Dkt. Msofe kuwa watahakikisha na vijiji 8 ambavyo bado havijajiunga vinajiunga na mradi huo.
"Tutahakikisha vijiji 8 ambavyo havijajiunga na mpango huo vinajiunga. Tutashirikiana kutoa elimu na nadhani kwa muda mfupi sana hao waliojiunga watakuwa mfano wa kusababisha wenzetu kutafakari upya na kujiunga na mradi huu." Alisema Dkt. Mashimba.
Aidha alieleza kuwa mradi umelenga kuwawezesha wananchi kupata manufaa kupitia wanyamapori kwenye vijiji vyao ambavyo vimekuwa vikikabiliwa na wanyamapori wakali na waharibifu hususani kwenye mazao na kusababisha hasara kubwa kwa wananchi.
Alieleza pia ili kuwezesha wananchi kufaidika na rasilimali za wanyamapori sheria imeelekeza kuanziasha WMA ili wananchi waweze kupata haki za matumizi ya rasilimali zote zinazowazunguka.
"Natumia fursa hii kuipongeza Wizara ya Maliasili na utalii kwa uwezeshaji wa mradi huu katika wilaya yetu ya Chamwino, aidha nawapongeza na viongozi wote wa Kata, Tarafa, vijiji na Wilaya kwa kuhakikisha mradi huu unakwenda kutelezwa vizuri." Alisema Dkt. Mashimba.
" Uwepo wa maeneo haya yanasaidia shughuli zote za kimila na kitamaduni kupata fursa kubwa kwa wawekezaji, hivyo ninawasihi sana viongozi wote na wananchiwa Wilaya tuendwlee kushirikiana ili kuwezeaha kufanikisha mirasi ya wizara hii, hususqni huu utekelezeke vizuri na tuhakikishe tunapata mafanikio makubwa kwenye Halmashauri yetu." Alisema Dkt. Mashimba.
Aliwaomba wananchi wanaporudi kwenye maeneo yao wasigeuke kuwa vikwazo vya kukwamisha mradi huu.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.