Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja ametoa wito kwa waheshimiwa Madiwani kusimamia mpango wa chakula shuleni na kuhakikisha wanafunzi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino hasa shule za msingi wanapata chakula
Mh. Janeth Mayanja ametoa wito huo leo Oktoba 29, 2024 wakati Akizungumza katika kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Wito huo umetolewa kufuatia kukosekana kwa chakula kwa baadhi ya madarasa katika shule za msingi hasa madarasa yasiyo katika mwaka wa mitihani hivyo kuwaomba waheshimiwa Madiwani kutekeleza mpango wa chakula shuleni kwa kuandaa mikutano na wazazi na walezi ili waweze kuchangia mpango wa chakula shuleni na kuwaelemisha faida za mwanafunzi kupata chakula shuleni kwani ni mmoja ya mpango wa lishe katika Wilaya ya Chamwino utakaowezesha kuepukana na tatizo la udumavu.
Sambamba na hilo, amewaomba waheshimiwa madiwani kuacha alama katika uongozi wao hasa katika eneo la chakula shuleni kwa kuhakikisha wanafunzi wote wanapata chakula kwani kwa kufanya hivyo watakua wamechangia maendeleo ya elimu kwa wanafunzi hao na kuchangia maendeleo katika jamii kwa ujumla
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mh. Janeth Mayanja amewaomba waheshimiwa Madiwani wote kuhakikisha wanatembelea miradi ya maendeleo mara kwa mara katika maeneo yao ili kutambua changamoto za miradi kwa ajili ya kuwasilisha changamoto hizo katika mamlaka husika ili kufanyiwa kazi pamoja na kuweka msukumo miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.