Shirika la Chakula Duniani (Word Food Programme-WFP) limekabidhi vifaa vitakavyosaidia kutambua hali ya udumavu wa mwili kwa watoto. Makabidhiano hayo yamefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Chamwino.
Mkurugenzi msaidizi wa WFP nchini Tanzania Bi. Wendy Bigham amemkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino vifaa vitakavyotumika kwenye ya vituo 65 vya kutolea huduma za afya (Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati)
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino Bw. A. H. Masasi ameishukuru WFP kwa kuipatia halmashauri vifaa hivyo na ushirikiano ambao umekuwa ukitolewa na shirika hilo katika mafunzo mbalimbali juu ya lishe. Aidha amesema vifaa vitasaidia katika kuboresha afya za watoto na kurahisisha utendaji kazi kwa watumishi wa afya katika kutoa ushauri kwa ajili ya lishe za watoto.
Akizungumza baada ya kupokelewa kwa vifaa hivyo Mganga Mkuu wa wilaya Dkt. Asteria Mpoto ameeleza kuwa kupitia vifaa hi to itasaidia kutambua uwiano sahihi wa udumavu kwa watoto katika hatua zao zote za ukuaji kwani kabla ya vifaa hivyo ilikuwa ni vigumu kupima urefu kwa watoto wasioweza kusimama.
"Kipimo hicho kitawasaidia wataalam wa afya kupata uwiano wa lishe na ushauri madhubuti kwa wazazi na walezi wilayani Chamwino. Awali ilikuwa ni vigumu kupata urefu sahihi kwa watoto wadogo, kwa kutumia kifaa hiki tunaweza kupimpa urefu hata wa watoto wenye umri mdogo zaidi" Alimalizia Dkt. Mpoto.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.