Mheshimiwa Naibu Waziri OR- TAMISEMI anayeshughulikia Masuala ya afya Mhe. Festo Ndugange amefanya ziara ya kikazi Wilayani Chamwino leo Desemba 05,2022.
Katika ziara hiyo amekagua shughuli mbalimbali zinazofanyika hospitali ya Uhuru na ameipongeza wilaya kwa kupata hospitali nzuri na amewapongeza watumishi kwa kufanya kazi vizuri.
"Ni hospitari nzuri yenye miundo mbinu bora, dhamira yake ni kuona wananchi wa Chamwino na Dodoma kwa ujumla wanapata eneo bora la kupata huduma za afya. Lakini pili niwapongeze kwa usafi, kwa kweli nimeridhishwa na usafi wa hospitali, mpangilio ni mzuri na watumishi wote tupo kazini".Amesema Naibu Waziri.
Vilevile Mhe. Waziri aliwapongeza kwa kuendelea na ujenzi wa miradi ya afya vizuri ana imani itakamilika kwa wakati ili yaanze kutoa huduma.
Alipongeza pia kwa vifaa tiba vingi ambavyo wamepewa na Serikali na katika hili aliongelea kuhusu mashine ya X - Ray ambayo imefungwa na kuanza kutumika na kusema kuwa hilio ni jambo jema ambalo litawaondolea wananchi adha ya kupatà huduma hizi mbali.
Vilevile alieleza kuwa wanajenga jengo la mtambo wa oxygen na linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi desemba mwaka huu ili,wagonjwa watakaokuwa na mahitaji ya oxygen waweze kupata hapa pasipokulazimika kwenda hospitali ya mkoa na maeneo mengine. Lakini pia kupunguza gharama kwa wananchi.
" kama mitambo hii ya oxygeni isipokuwepo hapa, kama mashine za xray zisingekuwepo hapa wangelazimika kwenda General hospitali ya mkoa, wangelazimika kwenda Benjamini Mkapa kwa ajili ya kupata oxygen au kupiga xray." Amesema Mhe Ndugange.
" Mhe. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta Chanwino mabilioni ya fedha lakini pia katika hospitali hii ya uhuru ili kuhakikisha vifaa hivi vinapatikana nawananchi wajirani wanapata huduma hapa". Amesema Mhe. Ndugange.
Aidha ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinafyata utaratibu uliowekwa na Serikali wa kutoa na kupokea dawa ili kueouka upotevu wa dawa. Vioeviie alielekeza kuhakikisha dawa zinapatikana kwa wagonjwa kwenye hisptali zote nchini kwa aslimia tisini na tano au asilimia mia moja
Mhe. Waziri aliwatia shime na kuwaekeza kuwa Mhe. Rais abatambua kazi kubwa inyofanywa na watumishi na ndio naana amelipa stahili mbalimbali walizokuwa wanadai na bado anaendelea kulipa. Vilevile amepandisha madaraja ya watumishi kwa kiasi kikubwa na kazi hio inaendelea.
Aliwaomba watumishi waendelee kufanya kazi nakuamini kuwa serikali itaendelea kuwaboreshea mazingira yakufanyia kazi. Aliomba wawe ba lugha nzuri kwa wagonjwa.
Kuhusu suala la gari la wagonjwa Mhe Waziri aliahidi kulishughulikia kwenye magari 300 ambayo Mhe Rais ametoa fedha yanunuliwe mojawapo litapelekwa hosp wanaiali ya Uhuru na nagari hayo yanatarajiwa kuwa yamefika mwishoni mwa mwezi desemba 2022 au mwanzoni mwa mwezi januari 2023.
"Hospitali hii ni kubwa na ipo barabarani naajali zibaweza kutokea wakati wowote na ndio maana wanefunga digital xray na hivyo awahakikishie OR - TAMISEMI wataieta gari ka wagonjwa." Amesema Mhe. Ndugange.
Kuhusu miundo mbinu alisema Serikali itaendelea kujenga majengo ambayo hayapo ili hospitali iweze kutoa huduma zinazotarajiwa.
Naye mganga mjuu wa mkoa dkt. Best Magoma alimshukuru Mhe. Waziri na kuahidi kutekeleza yote yaliyoagizwa na Mhe Naibu Waziri.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.