Na Brian Machange - Chamwino
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Kayanza Pinda amewataka wananchi wa Wilaya Chamwino kuongeza kasi ya kuhifadhi na kutunza mazingira kwa kupanda Miti kwa wingi katika maeneo ya makazi yao.
Ametoa kauli hiyo wakati akiongoza zoezi la upandaji miti Shule ya Sekondari Msanga Wilayani Chamwino, zoezi lililoratibiwa na Taasisi isiyo yakiserikali ijulikanayo kama "HABARI DEVELOPMENT ASSOCIATION" inayojumuisha Wanahabari Mkoani Dodoma.
"Tunapokata miti inachangia kukosekana kwa hewa safi, kwani uhai wetu unatokana na uwepo wa miti" Amesisitiza Mhe. Pinda.
Kwa upande mwingine Taasisi ya Habari Development Association umeushukuru Uongozi wa Halmashauri ya Chamwino pamoja na Shule ya Sekondari Msanga kwa kuwapa fursa na kuweka historia nyingine ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira ili kulifanya eneo lote la Msanga kuwa la kijani ukilinganisha mazingira yakijiografia ya Mji wa Dodoma.
Jitihada hizi zilizofanywa na Taasisi hiyo umewezesha upatikanaji wa miche ya miti takribani 5000 iliyopandwa katika eneo lote linalozunguka shule ya sekondari Msanga.
Wakati huohuo Mkuu wa shule ya Sekondari Msanga Mwl. Hatibu Luwumba ametumia fursa hiyo kumuomba Waziri Mkuu Mstaafu na wadau wengine wa maendeleo kuisaidia shule hiyo katika kuboresha miundombinu ya shule hiyo ilikuweka mazingira rafiki ya ujifunzaji na ufundishaji utakaowezesha kuinua taaluma ya shule hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.