Na Brian Machange - Chamwino, Dodoma
Waziri Mkuu leo Octoba 31, 2021 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za makazi zinazojengwa na shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika eneo la Chamwino, Dodoma.
akizungumza katika eneo hilo Waziri mkuu ameipongeza Wizara ya Ardhi pamoja na Shirika la Nyumba la Taifa kwa hatua ya ujenzi wa nyumba hizo pamoja na mpango wa ujenzi wa nyumba za makazi.
Pia amewapongeza wafanyakazi walioshiriki katika ujenzi huo ikiwa ni utekelezaji wa msisitizo wa mheshimiwa Rais Samia Suluhu hassan wa ushirikishwaji wa watanzania katika ujenzi wa miradi mikubwa ya ujenzi.
pia ametoa wito kwa NHC waweke mpango wa kuongeza nyumba hizo ikiwa zitajaa kutokana na uhitaji.
Ujenzi huo umehusisha nyumba 50 za vyumba vitatu vyenye ukubwa wa mita za mraba 125 pamoja na nyumba 40 za vyumba vitatu vyenye ukubwa wa mita za mraba 75.
Ujenzi wake unatarajiwa kukamilika ifikapo Disemba 2021 na kuanza kutumika ifikapo Januari 2022.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.