Na Brian Machange- CHAMWINO
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) ametoa siku 15 (kuanzia leo) kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa Wilayani Chamwino, Mkoani Dodoma.
Ametoa maagizo hayo leo Novemba 20,2020 alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, ambapo ameitaka Halmashauri ya Chamwino, Wakala wa Majengo (TBA) na Suma JKT kuhakikisha ujenzi wa Hospitali ya uhuru unakamilika ifikiapo Desemba 05, 2020.
Amesema Hospitali ya Uhuru ni moja ya miradi yakimkakati ya serikali ya awamu ya tano yakuimarisha utoaji wa huduma katika sekta ya Afya ambayo inaanzia kuboresha kuanzia ngazi ya Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya, Hospitali za Rufaa na Hospitali za magonjwa makubwa.
Mhe. Majaliwa amesema miradi ya kimkakati inatakiwa ikamilike kwa wakati na Watanzania wanahamu yakuona miradi hiyo inakamilika na kuanza kutoa huduma, hivyo fanyeni kazi kwa weledi ilikuweza kukamilisha ujenzi wa Hospitali hiyo muhimu kwa jamii.
Vilevile ametoa pongezi kwa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuweza kusimamia maeneo yote ya ujenzi wa miundombinu kwenye sekta ya Afya nchini kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita.
Awali akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru wilayani Chamwino, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema Hospitali ya Uhuru imekadiriwa kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 3.995 na kiasi kilichotengwa ni Bil3.410 ambapo zaidi ya shilingi Milioni 995 zilikuwa ni fedha za maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.