Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki , amezindua jengo la upasuaji na wodi ya wazazi katika kituo cha afya Dabalo wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo la upasuaji, wodi ya wazazi, vifaa tiba , vifaa na gari la kubebea wagonjwa katika kituo hicho.
Akizungumza katika hafla hiyo mei 09, 2023, amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za afya kwa kuwasogezea huduma hizo karibu na makazi yao.
“Ndugu zangu Mhe. Rais wetu kila mara anaendelea kupambana kuhakikisha anaendelea kukazania vipaumbele vyake, nchi yetu inamahitaji makubwa na mmeona ni kwa namna gani ndani ya muda mfupi ameendelea kuweka mkazo katika kushughulikia vipaumbele mablimbali ikiwemo kuweka huduma karibu na wananchi, ”Alisema Waziri Kairuki.
“Mmeona ni kwa namna gani kwa sekta ya Afya jinsi ambavyo ameweka kipaumbele katika utoaji wa huduma za afya lakini vilevile sio huduma tu pia kuhakikisha kwamba hata zile gharama zinazotozwa basi zinakuwa ni gharama ambazo kweli wananchi wetu wanaweza kuzimudu”, alisema.
Mhe. Angellah Kairuki amelishukuru shirika la Umoja wa Mataifa linaloshugulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) kupitia mradi wa kuboresha huduma za afya ya uzazi , watoto na vijana (RMNCAH – UFPA) iliyofadhiliwa na serikali ya Denmark
“Nipende pia kuwashukuru shirika la Umoja wa Mataifa linaloshugulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) kupitia mradi wa kuboresha huduma za afya ya uzazi , watoto na vijana (RMNCAH – UFPA) iliyofadhiliwa na Serikali ya Denmark kwa namna ambavyo wameendelea kutoa huduma mbalimbali na misaada katika sekta ya afya na sekta nyingine ,”alisema.
“Hii inaonyesha ni namna gani wanayo dhamira na wajibu wa kuendelea kushirikiana na kuunga mkono jitihada na juhudi mbalimbali za Serikali na hasa katika kuwafikia wananchi wetu wa Tanzania na hususani walio achwa nyuma na huduma bora za afya,” alisema Waziri Kairuki
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.