Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo, ameitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Uhuru iliyoko Wilayani Chamwino na kuonesha kukerwa na baadhi ya watendaji wa serikali kubeza matumizi ya mfumo wa ‘Force Account’ kwenye masuala mbalimbali ikiwemo ununuzi wa vifaa kwenye majengo ya serikali.
Kero hiyo ya Waziri Jafo ilitokana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binnilith Mahenge kumweleza kuwa Mkandarasi kutoka Kampuni ya Suma JKT ambayo niwatekelezaji wa mradi huo kueleza kuwa baadhi ya vifaa kuchelewa kuwekwa kutokana na gharama zake kuwa juu.
“Unaenda Suma JKT unakuta milioni moja na laki nne, unaenda Don Bosco kule milioni moja na laki mbili lakini unaenda kwenye masoko unakuta laki sita na nusu halafu unasema taratibu za manunuzi, hii haikubaliki katika utendaji nakuagiza Mkurugenzi nenda kanunue vifaa kwa gharama ya soko” amesisitiza Waziri Jafo.
Waziri ameeleza kuwa, anakerwa na baadhi ya watu wakiwemo viongozi wanaokashifu utaratibu wa "Force Account" unaondoka site unakuta kitu kinauzwa laki sita halafu huku unapata milioni moja na laki nne au mbili kwanini usiende kununua pale pa bei rahisi?
Waziri Jafo amefafanua kuwa, Rais Magufuli amajenga vituo vya Afya 487 kwa utaratibu wa "Force Account" na kwamba mwanzo kwa kutumia kandarasi za mwanzo majengo yalikuwa yanajengwa kwa fedha nyingi na gharama kubwa.
“Naomba viongozi wenzangu wengine mnaokaa mnakashifu utaratibu wa Force Account msiongopewe hivi hamfikirii zamani jengo la Bilioni mbili leo linajengwa kwa bei ndogo halafu leo watu wanasimama wanasema utaratibu huu hauna maana unajua kuna watu wa ajabu sana na inawezekana hawajui maisha halisi ya watanzania huu utaratibu umetusaidia shule kongwe zimekarabatiwa” amesema Waziri Jafo.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Mahenge alimweleza Waziri huyo kuwa mradi ulikuwa uwe umekamilika lakini kuna changamoto ya baadhi ya fedha ambazo bado hazijatolewa.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.