Mheshimiwa waziri wa Kilimo Hussen Bashe amefanya uzinduzi wa usajili wa wakulima na mwongozo wa utoaji wa ruzuku ya mbolea msimu wa 2022/2023 ambao utafanyika kidigitali.
Uzinduzi huo ameufanya leo Julai 4, 2022 kwenye ukumbi wa Serikali ya kijiji cha Chamwino Wilayani Chamwino. Katika uzinduzi huo Mhe Bashe aliongozana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. David Silinde. Viongozi wengine waliohudhuria ni Katibu Mkuu na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Wakuu wa Wilaya wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawemameneja wa VODACOM na Benki ya CRDB na Mkurugenzi mtendaji toka TFRA.
Katika uzinduzi huo Mhe. Waziri ameeleza kuwa Serikali imeshanunua mashine za kupima udongo143 ambazo zitagawiwa kwenye Halmashauri zitakazotumika kupima afya ya udongo kwenye mashamba ya wakulima na baada kupima mkulima atashauriwa eneo lake linapaswa kulima mazao gani au atumie virutubisho gani au mbolea itakayoendana na eneo lake. Na akishapimiwa atapewa cheti kitakachoonyesha matokeo ya kipimo.Aidha ameeleza kuwa huduma hio itatolewa bure.
Vilevile Mhe. Waziri ameeleza kuwa Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan anaumizwa na umasikini wa watu wa Tanzania. Kokote anakozungumza utasikia akizungumzia kuboresha kilimo na kuondoa umasikini. Na Mhe. Rais hajaishia tu kusema, ukichukua bajeti ya kilimo ya mwaka huu wa fedha ni zaidi ya shilingi tilioni moja na haijakwenda kwenye posho wala vikao.
Mhe. Waziri pia ameeleza kuwa kwenye sherehe za nanenane mwaka huu Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan atashuhudia utiaji saini wa mikataba ya umwagiliaji yenye thamani ya bilioni 400 ambazozitakwenda kujenga skimu za umwagiliaji.
Vilevile Mhe. Waziri ameeleza kuwa Serikali imetenga kiasi cha shilingi ilioni 150 kwa ajili ya ruzuku ya mbolea kwa wakulima.
Katika mapinduzi ya kilimo Wizara imepanga imepanga kufanya kilimo cha mfano cha mashamba makubwa (block farming) kwa mkoa wa Dodoma katika Wilaya ya Chamwino na Bahi ambapo jumla ya zaidi ya hekta elfu 23, na kwa Chamwino pekee zimetengwa hekta elfu 20 na mashamba haya yanakwenda kuajiri vijana, na wataanza na kilimo cha alizeti na watapewa umiliki wa miaka 30 adi 60 juu ya umiliki wa hati kuu. Na kwa block tatu za Chamwino moja ya kata ya Membe yenye hekta 8000 itakuwa ya skimu ya umwagiliaji.Katika uzinduzi huo Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Isaya Msuya alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.