Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imefanya Mkutano maalum wa kuunda Jukwaa tendaji la Kilimo, Ufugaji na Ardhi lenye lengo la kuwakutanisha Wakulima na Wafugaji ili iwe rahisi kuwahudumia.
Mkutano huo maalum umefanyika katika ukumbi wamikutano wa Halmashauri leo Agosti 4, 2023 ambapo umeshirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na wakulima na wafugaji.
Akizungumza alipokuwa anafungua mkutano Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya Dkt. Semistatus Mashimba amesema Jukwaa watakalounda litasaidia kuzungumzia changamoto za wakulima na wafugaji pamoja na kuzitatua.
" ninafahamu wakulima, wafugaji wanachangamoto nyingi, lengo la jukwaahilo ni kuhakikisha sisi kama Serikali tunawakutanisha na hawa watu wanaotatua changamoto zenu. Zipo Taasisnyingi zinapiga simu ofisi ya Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya zinasema zinataka kusaidia wakulima na wafugaji na wamojawapo ni mradi wa kuwainua wanawake UN WOMEN na siyo Taasis tu hata Serikali." Alisema Mkurugenzi.
Wajumbe wameweza kuchangia mawazo yao kwenye Rasimu ya Katiba ya Jukwaa tendaji la Kilimo, Mifugo na Ardhi na wote kwa pamoja walikubali kuundwa kwa Jukwaa hilo pamojà na kupitisha rasimu ya katiba.
Uzinduzi wa Jukwaa hilo unatarajiwa kufanyika Agosti 25, 2023 kwenye Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Akizungumza kwenye uundaji wa Jukwaa Mwenyekiti wa wafugaji John Kochocho amempongeza Mkurugenzi kwa maono yake ya kuanzisha Jukwaa na kuwasihi wafugaji wenzake kujiunga nalo kwani linafaida kubwa kwao.
"Nakupongeza Mkurugenzi kwa jambo ulilolifanya la kuunganisha wakulima na wafugaji kwa kuwa huwawanachangamoto sana na wanashindwa watazipitisha wapi. Ninaimani hili jukwaa wakulima na wafugaji litakuwa kimbilio lao",alisema mwenyekiti wa wafugaji.
" Sisi huwa hatuamini kitu mpaka uone mwenzako ameingia, ingia utaona faida. Faida yake kwenye kupimiwa ardhii, lakini hata kututafutia masoko ya mifugo. Hakuna mfugaji masikini, mbuzi mmoja tu kwa sasa anauzwa karibu shilingi laki moja." Alisema Mwenyekiti wa wafugaji.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya amepongeza uundwaji wa Jukwaa hilo na kusema litaondoa migogoro ya wakulima na wafugaji nakuwaomba wakulima na wafugaji kujiunga na chombo hicho kwani kiingilio wamekiweka wao wenyewe.
" Tunapozungumzia migogoro ya wakulima na wafugaji tuliyonayo hiki chombo ndio kitakwenda kuimaliza", alisema Mwenyekiti.
Vilevile amezielekeza taasis za benki hususani NMB kuona ni namna gani watatoa mikopo kwa wakulima na wafugaji watakaokuwa wamepimiwa ardhi zao na TRA baadae Jukwaa litakapoanza waeleze ni kwa namna gani watasajili mifugo na wakulima ili wawezkupata mikopo kwenye vyombo vya kifedha.
Wadau waliosaidia katika shughuli ya uundwaji wa Jukwaa ni pamoja na UN WOMEN, NMB Benki, CRDB Benki, TOAM, PBZ Benki
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.