Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wametakiwa kutangaza mazuri yanayofanywa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Agizo hilo limetolewa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Ndugu Pilli Mbaga Novemba 15, 2023 wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma ya kukaguwa miradi ya maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi Wilayani Chamwino.
"Bado mna kazi kubwa viongozi wa Chama kwenda kusema yale mazuri yote yanayoletwa kwenye kata yetu, tukaseme miradi iliyoletwa hapa. Kama kuna zahanati tukaseme zahanati zimejengwa, madarasa yamejengwa. Tuwahabarishe wananchi wawe na taarifa hizo." Alisema Katibu.
Alisisitiza kuwa jambo kubwa ni kwenda kufanya mikutano ya hadhara, mkawaambie miradi iliyopo.
"Niwaombe sasa viongozi wa Chama na viongozi wa Serikali na Mhe. Diwani, kazi kubwa uliyonayo sasa ni kufanya mikutano ya hadhara kwenye mitaa ili kuwaambia wananchi yale yote yanayofanywa na Mhe. Rais na miradi yote iliyokuja kwenye kata yako ili waweze kifahamu." Alisema Katibu.
Vilevile alisisitiza viongozi waendelee kukagua utekelezaji wa ilani na hapo watakuwa wamemuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi anazozifanya za kuweza kuleta miradi mingi na fedha nyingi.
Mradi iliyokaguliwa na Kamati ya siasa Mkoa wa Dodoma ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya ya mfano ya wasichana ya Mkoa wa Dodoma iliyopo kata ya Manchali, ujenzi wa mabweni shule ya Sekondari ya Chilonwa iliyopo kata ya Chilonwa, Kituo cha afya Dabalo kilichopo kata ya Dabalo, ujenzi wa shule mpya ya Msingi Kwahemu iliyopo kata ya Haneti, mradi wa maji Iringa Mvumi uliopo kata ya Iringa Mvumi na ujenzi wa shule ya msingi Mjeloo yenye mikondo miwili iliyopo handali.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.