Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma toka Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi wamesheherekea siku ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kujitolea Damu katika Hospitali ya Uhuru iliyopo Wilayani Chamwino Mkoani dodoma
Katika zoezi hilo lililofanyika Hospitalini, hapo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Dokta E. Kessy amesema kuwa Chupa 48 za Damu zimepatikana kwenye maadhimisho hayo.
Nao wanafunzi hao wakiongea kwa nyakati tofauti tofauti wamesema kuwa Wameona vyema kushiriki maadhimisho ya Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kujitolea Damu katika hospitali hiyo ikiwa ni ishara ya kuunga juhudi kubwa zinazofanyawa na Rais wa Awamu ya Tano Dr. John Joseph Magufuli katika kuinua sekta ya Afya nchini.
Awali, kabla ya zoezi hilo la kujitolea Damu kulitanguliwa na zoezi la upandaji miti pembezoni mwa hospitali ya Uhuru zoezi lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma wakishirikiana na Viongozi toka Halmashauri ya Wikaya ya Chamwino.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.