Hospitali ya Wilaya Inayojengwa Kutowanufaisha Wananchi
Mheshimiwa Livingstone Lusinde Mbunge wa jimbo la Mtera Wilaya ya Chamwino ameyasema hayo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya.
Mhe. Lusinde alisema mbali na hospitali hiyo kupendekezwa kujengwa Kata ya Chamwino ambapo tayari kuna Kituo cha Afya, lakini pia mgawanyo (jiografia) wa Wilaya hiyo hauko vizuri kwani popote pale itakapojengwa Hospitali hiyo ya Wilaya katika Majimbo yote mawili haitoweza kuwanufaisha wananchi Wote waliopo ndani ya Wilaya.
Jambo ambalo liliungwa mkono na Waheshimiwa Madiwani wengine na kueleza kuwa ili wananchi waweze kupata huduma bora zinazokidhi, Wilaya hiyo inapaswa igawanywe .
Akijibu hoja hiyo Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndugu Athumani Hassan Masasi, alisema kwa mujibu wa sheria majengo yote ya Serikali yanapaswa kujengwa makao makuu ya Wilaya. Aidha alieleza kuwa uwepo wa Kituo cha Afya hauzuii kuwepo kwa Hospitali ya Wilaya hivyo aliendelea kushauri kuwa ujenzi huo uendelee kwa eneo lililopendekezwa.
Kutokana na mjadala huo Waheshimiwa Madiwani walitoa Maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji Wilaya kukaa na menejimenti na kuiandikia Mamlaka husika kuhusu pendekezo la kuigawa Wilaya hiyo ili kuleta tija katika kuwahudumia Wananchi.
Aidha taarifa ilitolewa kuwa katika kipindi hiki cha robo ya kwanza cha Julai hadi Septemba Halmashauri imetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa fedha zilizopokelewa katika robo hii pamoja na fedha zilizovuka mwaka 2017/2018 ambapo jumla ya Shilingi 7,427,214,762.000.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.