Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gifty Isaya Msuya, amewapongeza Ofisi ya Takwimu ya Taifa kwa kuwasilisha matokeo ya sensa kwa ngazi ya wilaya na kata.
Pongezi hizo amezitoa wakati wa uwasilishwaji na utoaji wa takwimu katika wilaya ya Chamwino iliyofanyika, 28 juni 2023 wilayani hapo.
“Niwapongeze kwa zoezi hili mmetoa ushirikiano zaidi kwa kufanikisha zoezi hili, ndugu zangu wanachamwaino niwaambie jambo moja sisi Chamwino na mkoa wa Dodoma tunabahati kubwa sana kwa sababu uzinduzi wa muongozo wa sensa umefanyika hapa Dodoma, lakini uzinduzi wa kwanza wa matokeo ya sensa Tanzania yamefanyika hapa Dodoma, lakini pia uwasilishaji wa namna hii ya kuwaita viongozi wote wa vijiji, kata mpaka chini imefanyika mkoa wa Dar es salaam na Dodoma,”
“Hii inaonyesha sasa tukae mguu sawa kwakuwa mambo mazuri yanakuja lakini niwaombe sana taarifa zilizotolewa za matokeo zinasema kwamba matokeo ya vijiji na vitongoji yamesha chakatwa lakini yanasubiri taratibu ya kuzinduliwa na kutumika”, alisema Mkuu wa Wilaya.
Kwa sasa wilaya ya Chamwino kwa mujibu wa takwimu za sensa ya watu na makazi ya 2022 inajumla ya idadi ya watu 486,176
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.