Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa kushirikiana na wadau wa TCI wakishilikiana na Jhpiego wametambulisha mradi utakaohusumasuala ya uzazi wa mpango.
Mradi huu umezinduliwa Desemba 13, 2022, kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Mradi huu umetambulishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Chamwino pamoja na Wakuu wa Idara wa Halmashauri.
Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa shirika la Jhpiego Tanzania Bibi Rose Mzava anesema mradi huu unatekeoezwa katika mikoa nane Nchini ukiwemo mkoa wa Dodoma. Kwa mkoa wa Dodoma walianza na Halmashauri ya jiji la Dodoma na sasa wanaanzisha Chamwino.
Akizungumza alipokuwa anafungua kikao nwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ndugu Mohamed Mfaki amesema wameupokea mradi huo kwa asilimia mia moja. Aliwaomba wakuu wa Idara kutoa ushirikiano na kuyapokea maelekezo yatakayotolewa kwa umakini ili mradi uwe na tija.
Vilevile aliwaomba kupekeka elimu kuhusu mradi huu kwa wananchi pamoja na kupeleka !huduma rafiki kwa vijana.
Kwenye utambulisho huo wajumbe waliweza kujadili na kuuliza maswali mbalimbali kuhusu mradi na maswali yote yaliweza kujibiwa.
Naye Mratibu wa mama na mtoto (RCH) wa Halimashauri ya jiji la Dodoma alitoa ushuhuda wa jinsi wanavyotekeleza mradi huo kwenye Halmashauri yao na mafanikik ambayo tayari wameyapata.
Mwisho wajumbe waliombwa na Bibi Mfalila msimamizi wa mradi kwa mkoa wa Dodoma kujitokeza kwa hiari kwa ajili ya kuwa ma 'focal person' wa mradi ambapo walijitokeza watumishi watano, Hàppy Mgongo kutoka Idara ya Elimu msingi, Raymond Mahugi kutoka Idara ya Mipango, Zena Ibrahim kutoka Idara ya Usafi na udhubita wa taka, Nicholaus Achimpota kutoka idara ya utamaduni, saana na michezo na Mtemela kutoka Idara ya Ujenzi
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.