Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Chamwino Dkt. Semistatus H. Mashimba amefanya mkutano na wananchi wa kitongoji cha Mwongozo kilichopo kata ya Chamwino Septemba 1, 2022 ambao eneo lao litapangwa, kupimwa na kutwaliwa na Serikali kwa ajili ya maendelezo ya mji.
Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Serikali ya kijiji cha Chamwino ambao ulihudhuriwa na wananchi wa kitongoji cha Mwongozo na viongozi wa kijiji na kata ya Chamwino.
Lengo la mkutano huo ni kutoa elimu kwa wananchi ili kuondoa sintofahamu iliyokuwepo ambapo wananchi walidai kuwa Serikali inapima eneo hilo ili iwafuze kwenye maeneo yao. Aliomba wasitafsirke vibaya kazi yao ni kupanga na kupima.
"Naomba tusitasirike vibaya kazi yetu sisi ni kupanga na kupima , hatumnyang'anyi mtu ardhi. Kuna dhana kwamba tunataka kufukuza watu, hiyo anaikana. Wanachotaka ni kupima na kumilikisha".
Akiongea kwenye mkutano huo Mkurugenzi alieleza kuwa lengo la kupanga, kupima na kutwaa eneo hilo ni kwa ajili ya kuupanga mji wa Chamwino ili uwe na matumizi bora ya ardhi. Kumekuwa na maswali mengi yanaulizwa kwa nini Chamwino haipimwi, kwa nini inamapori mengi na kwa nini vitu vya maendeleo haviwekwi .
" Imeonekana Chamwino watu wengi wanahodhi maeneo ili baadae wazuie shughuli za maendeleo. Hivyo watafanya uhakiki wa maeneo ya Chamwino ili wote wanaomiliki maeneo watambulike kwa majina na kwa plot. Wakikuta unamaeneo kitongoji A, B na C au Buigiri watachukua hatua kwani watu wanahodhi maeneo kwa manufaa binafsi. Hawataki Serikali ipange vizuri matumizi ya ardhi. Wanajimilikisha ardhi ili baadae waanze kudai fidia".
Aidha alieleza kuwa mahali popote duniani sehemu inapokuwa Ikulu kuna taratibu wake wa kupanga . Huwezi kuwa na Ikulu halafu pembeni yake kunakuwa na vibandabanda. Hivyo kuna mambo ya usalama na hadhi pia.
Alieleza kuwa watapima atakaekubali kulipwa fidia atalipwa na atakayekataa atatoa sababu kwa nini hataki kulipwa fidia.
Naye mtaalam kutoka ofisi ya ardhi alieleza kuwa sheria ya ardhi inasema ardhi yote ya Tanzania ni mali ya Watanzania lakini inasimamiwa na Mhe. Rais na hapa Chamwino Mkurugenzi ni mteuliwa wa Mhe. Rais naye pia anajukumu hilo la kusimajia masuala ya ardhi.
Vilevile alieleza kuwa suala la kutwaa ardhi ni kwa ajili ya maslahi ya umma na maslahi ya umma ni uwepo wa huduma za kijamii. Na hakuna viwanjavinapangwa na kupimwa pasipokuwa na huduma za jamii. Hivyo wanaitwaa ardhi hiyo kwa ajili,ya kuweka huduma za jamii na maendelezo ya mji.
Aidha mtaalaju wa ardhi alieleza kuwa katika kutwaa ardhi sheria haiko kwa ajilimya kumtajirisha mwananchi bali ni kufuata bei ambayo haitamuujiza mwananchi wala kuimiza Serikali. Kutwaa ardhi ni suala la kisheria, na kukataa ardhi isitwaliwe ni kupingana na sheria. Na mtu anapopinga sheria kuna taratibu za kufuatwa.
Wizara ya ardhi imewezesha fedha kwa ajili ya kupanga mji huu ambao ni makao makuu ya Nchi.
Aliendelea kusema kuwa kuna maeneo mengine watafanya upimaji shirikishi kwa kugawana viwanja vitakavyopatikana na ili kuondoa migogoro ya ardhi ni lazima wawamilikishe maeneo yao.
Baada ya maelezo hayo wananchi waliwasilisha hoja zao na hoja mojawapo ilikuwa kuhusu suala la fidia ambapo walieleza kuwa Halmashauri ya Chamwino fidia zake zimekuwa zikilipwa ni ndogo ukilinganisha na maeneo mengine ya Dodoma. Wananchi walipendekeza walipwe fidia ya shilingi milioni nne kwa kila ekari moja.
Ufafanuzi ulitolewa nw mtaalamu wa ardhikuwa bei ya fidia ya ardhi inalipwa kulingana na bei ya soko. Eneo litalipwa fidia kulingana na vitu watakavyovikuta kwenye eneo. Sheria pia haizuii kwa wale ambao wametoa maeneo kama watakuwa wanahitaji viwanja kupewa viwanja badala ya fidia ya fedha.
Naye Mkurugenzi Mtendaji alieleza kuwa wamemuomba Mthamini kutoka ofisi ya Kamishina wa Ardhi awaongeze walau isiwe chini ya shilingi milioni tatu, ili shilingi milioni moja ilipwe kama fedha ya usumbufu( disturbance allowance ). Kuhusu kulipwa shilingi milioni nne hilo watajadiliana na Mthamini pindi atakapokuja.
Katika mkutano huo wananchi walikubaliana kazi hiyo ianze tarehe 2 Septemba 2022 kwa kupanga eneo na kuwaelimisha wananchi kila eneo limepangwa kwa ajili ya huduma gani.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.