Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli ameridhishwa na hali ya usalama na ufanyaji wa mitihani ya darasa la Saba Mkoani Dodoma.
Ameyasema hayo leo wakati alipotembelea baadhi ya shule za msingi mkoani Dodoma kwa ajili yakujionea hali halisi ya mazingira yakufanyia mitihani ya kumaliza Elimu ya msingi.
Mweli amesema kuwa lengo lakutembelea shule hizo nikuona taratibu zote za ufanyaji mitihani zinafuatwa na hali ya usalama wa mazingira yakufanyia mitihani inaridhirisha ili kuhakikisha mitihani hiyo inakamilika katika hali ya amani na utulivu nchi nzima.
Amesema kuwa ameridhirshwa na maandalizi,mazingira na utulivu wa wanafunzi katika shule hizo hali ambayo inatoa matumaini kwa wanafunzi kufanya mitihani yao katika mazingira salama na yenye utulivu mkubwa.
‘Nipongeze Uongozi wa Mkoa wa Dodoma kwa maandalizi mazuri ambayo yamewezesha wanafunzi kufanya mitihani yao ya kumaliza Elimu ya msingi katika mazingira bora yenye amani na utulivu’ Amesisitiza Mweli.
Amewataka wasimamizi wa mitihani kote nchini kuendelea kufuata sheria,taratibu na miongozo ya usimamizi wa mitihani kwa kuhakikisha wanafunzi wanafanya mitihani yao bila usumbufu ili mitihani hiyo iweze kukamilika kwa amani na utulivu.
Aidha ametoa wito kwa wasimamizi walioteuliwa kufanya kazi yao ya usimamizi kwa umakini na uadilifu kwa kuzingatia kanuni za mitihani na miongozo waliopewa kwakuwa mitihani ni eneo muhimu sana katika upimaji uelewa wa wanafunzi.
Wanafunzi milioni 1,024,007 wanatarajiwa kufanya mitihani ya kumaliza Elimu ya msingi kati yao wavulana ni 493,289 sawa na asilimia 48.17 na wasichana 530,718 sawa na aslimia 51.83.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.