"Serikali ya awamu ya sita imepanga kufanya mabadiliko makubwa kwenye sektamya mifugo."
Hayo yamesemwa kwenye ufunguzi wa mafunzo rejea kwa maafisa ugani Nchini kwa kanda ya kati yanayofanyika Wilayani Chamwino kwa siku mbili, Novemba 14,2022.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Waziri wa mifugo na uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki amesema sekta ya mifugo inawategemea maafisa ugani katika kuleta matokeo chanya japokuwa wapo wachache. Alieleza kwa uchache wao huohuo kama watakipenda wanachokifanya watafanikiwa.
" Sekta ya mifugo kwa matokeo chanya tunawategemea ninyi. Ninyi ndio askari wa mstari wa mbele ili kuleta mafanikio." Alisema Mhe. Ndaki.
"Kwa mpango huu wa mabadiliko tunaweza kuleta mabadiliko ya mtu mmoja mmoja. Aliongeza kusema kuwa sekta ya mifugo kwa kiasi kikubwa imetawaliwa na ufugaji wa asili na tukiendelea na na tukiendelea na uasili huu hautatufikisha mahali pazuri." Alisema Mhe. Ndaki.
Aidha Mhe. Waziri Ndaki alieleza kuwa kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 sekta ya mifugo inakuwa kwa 7% . Aliendelea kusema kwa idadi ya mifugo tuliyonayo tungefuga kwa tija tungeweza kuishi kwa kutegemea ng'ombè tu. Lakini kwa sasa unakuta ng'ombe wanauzito mdogo jambo linalopelekea kuwa na tija kidogo na maziwa machache.
Mhe. Ndaki alieleza kuwa kwa mwaka huu wa fedha wamepanga kufanya nafunzo kwa ngazi zote kwa wataalamu na wafugaji. Alisema tukiwaelimisha wafugaji wetu itakuwa chanzo cha kuwabadilisha ili wafuge kwa tija.
Vilevile Mhe. Waziri alieleza kuwa kupitia mpango wa maboresho wameanzisha vituo atamizi kwa vijana ambapo vijana 240 waliohitimu masuala ya mifugowamesajiliwa kwenye vituo hivi. Lengo likiwa ni kutengeneza wafugaji wa leo na kesho ili kuwa na wafugaji wenye tija.
Alieleza kuwa wanamshukuru Mhe. Rais mama Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia bl. 5 kuwezesha vituo hivyo na mradi huo wameuita "Samia Ufugaji Programme". Baada ya mwaka mmoja watafuzu na kuondoka na kuita watu wengine.
Kuhusu changamoto ya vitendea kazi Mhe. Ndaki alieleza kuwa tayari wameshagawa pikipiki 300 na kwa mwaka huu wa fedha watatoa pikipiki 1200 na magari 13 kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa.
Katika kufikia maboresho Wizara imeanzisha mfumo ( M - kilimo na Ugani kiganjani) ambayo itawezesha Wizara kupokea taarifa moja kwa moja toka kwa maafisa ugani na alitoa rai kwa ambao hawajajisajili wajisajili. Aliagiza wafugaji pia wasajiliwe kwenye mfumo.
"Tumeanza mifumo ya usimamizi wa huduma za mifugo ( M - kilimo na ugani kiganjani) kupitia mifumo hii Wizara itapata taarifa moja kwa moja toka kwenu." Alisema Mhe. Waziri.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.