RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan azindua zoezi la uandikishaji wa daftari la mpiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa leo Oktoba 11, 2024 katika Kijiji cha Chamwino, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Mh. Rais amezindua zoezi hilo kwa kujiandikisha katika daftari la mpiga kura uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika kitongoji cha Sokoine, Kijiji cha Chamwino.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo amewaasa wananchi wote kujitokeza kujiandikisha ili kuchagua viongozi wa kijiji na kitongoji ili kupata haki yao ya kikatiba pamoja na kutochanganya kati ya zoezi la kujiandikisha katika daftari la mpiga kura wa uchaguzi Serikali za Mitaa pamoja na kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpira kura kwa uchaguzi wa mwaka 2025 ambalo limetangulia katika Wilaya ya Chamwino.
Katika uzinduzi huo amesema pia uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni muhimu kwani viongozi wa Vijiji na Vitongoji husaidia kuhakikisha usalama katika maeno yao unapatikana kwa kusaidia kutambua wakazi wa maeneo yao. Pia husaidia kukuza maendeleo kuanzia ngazi ya Vitongoji na Vijiji.
Aidha, Mh. Dtk. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kuhakikisha wanachagua viongozi wapenda maendeleo na watakaopeleka maendeleo katika maeneo yao. Pia amewaasa wananchi kuhakikisha zoezi la uandikishaji wanalifanya kwa usalama kwani ndilo huleta taswira ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Zoezi la kuandikisha orodha ya wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa limeanza leo Oktoba 11, 2024 na kutamatika tarehe 20 Oktoba 2024.
Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.