Chamwino Yapongezwa Kwa Kuongeza Ufaulu Wa Darasa La Saba
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Billinith Mahenge ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa kuongeza ufaulu wa darasa la saba kutoka asilimia 54 hadi kufikia asilimia 64.
Pongezi hizo amezitoa hivi karibuni alipofanya ziara ya kukagua shughuli za kilimo pamoja na ujenzi wa miundombinu ya madarasa ambayo yanapaswa kujengwa baada ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 kukosa madarasa ya kusomea kutokana na ongezeko la ufaulu .
Akizungumza katika kikao Mkuu wa Mkoa alitaka kufahamu katika upungufu wa vyumba 30 vya madarasa ni vyumba vingapi ambavyo vimekamilika.
Afisa Elimu Sekondari Wilaya ndugu David Mwamalasi alieleza kuwa vyumba vya madarasa 14 tayari vimekamilika.
Aidha Mkuu wa Mkoa ameahidi kuchangia kuchangia tofali kwa vyumba vitatu vya madarasa ambapo vyumba viwili vitajengwa shule ya Sekondari Buigiri na chumba kimoja shule ya Sekondari Chamwino na wananchi wachangie mchanga na mawe.
Vilevile ameagiza kuwa kazi ya ujenzi wa madarasa kwa maeneo ambayo hayajaanza kujenga ianze mara moja na kukamilika ndani ya mwezi huu ili wanafunzi waanze masomo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.