Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Staki Senyamule, amewapongeza wanafunzi wa kidato cha sita Shule ya Sekondari Chilonwa kwa kupata ufaulu mzuri katika mtihani
Mkuu wa Mkoa amehudhuria hafla iliyoandaliwa na benki ya NMB kwa ajili ya kumkabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya shule za msingi na Sekondari pamoja na vituo vya kutolea huduma za Afya ikiwa ni sehemu ya benki kurudisha kwa jamii. Hafla imefanyika shule ya msingi Mizengo Pinda Julai 19, 2023.
Akiongea kwenye hafla hiyo meneja wa kanda ya kati wa NMB Bibi Janeth Hango amesema vifaa vilivyotolewa ni mabati 88 na misumari kwa ajili ya shule ya sekondari ya makang'wa yenye thamani ya tsh 4900,000/= .mabati 111, mbao 227, misumari na waya kg 110 kwa ajili ya shule ya msingi Mizengo Pinda vyenye zaidi ya shilingi milioni 10, mabati 95, mbao 245, misumari pamoja na waya kg 178 kwa ajili ya shule ya msingi Chinangali vyenye thamani ya tsh. Milioni 5.
Vifaa vingine vilivyotolewa ni mabati 160 misumari kg 135 na kofia za mabati 15 kwaajili ya shule ya msingi Dabalo vyenye thamani ya shilingi milioni 6, mabenchi 60 na makabati 6 ya maabara kwa ajili ya shule ya sekondari Buigiri vyenye thamani ya shilingi milioni 5. Vifaa hivyo vyote vimegharimu jumla ya kiasi cha shilingi milioni arobaini na tatu (43).
Akizungumza kwenye hafla hiyo mkuu wa mkoa ambaye alikuwa mgeni Rasmi amempongeza Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kufanya mapinduzi makubwa kwenye sekta ya Elimu akitolea mfano ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano, ujenzi wa shule mpya za sekondari, shule mpya ya mfano ya wasichana ya mkoa wa Dodoma na chuo cha VETA ambavyo vyote vinajengwa wilayani Chamwino.
Mkuu wa mkoa pia ameipongeza benki ya NMB kwa kuona umuhimu kwa kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuchangia vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 43 na kauli mbiu ya Mhe. Rais anayosema elimu, afya na mazingira wameona watembee nayo. Kipekee ameshukuru kwa kuamua kuleta misaada hiyo Dodoma na hususani Chamwino ambapo kulikuwa na uhitaji mkubwa.
Amewapongeza pia wanachi kwani wao ndio walioanzisha ujenzi wa shule ya Mizengo Pinda. Alitoa wito kwa wanachi wa Dodoma kuendelea kuanzisha miradi kwani wadau huchangia sehemu ambayo imeshaanzishwa na kuhitaji uksmilishaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.