Mwenge wa Uhuru Wilayani Chamwino umepitisha miradi yote sita iliyopangwa kutembelewa ambapo kati ya hiyo miradi mitatu ilizinduliwa, miradi miwili kuwekewa mawe ya msingi na kutembelea mabanda ya vikundi na kukabidhi hundi kwa kikundi cha vijana.
Katika mradi wa uzinduzi wa chanjo ya mifugo, uogeshaji na uvalishaji hereni kwa mifugo ilielezwa kuwa wanyama waliotambuliwa mpaka sasa ni ng'ombe 18,678, mbuzi 7,445, kondoo 2,797 na punda 237. Ambapo lengo la mradi ni kudhibiti magonjwa ya mifugo, utambuzi wa mifugo na kukuza kipato kwa wafugaji.
Aidha ilielezwa kuwa mradi utawezeaha kupunguza vifo vya mifugo na kuongezeka kwa mifugo, kuongezeka kwa kipato kwa wafugaji kutokana na kuongezeka kwa mifugo iliyo bora. Kurahisisha biashara ya mifugo na mazao yake wilayani, ndani na nje ya nchi. Kuwezesha wafugaji kupata mikopo na kuweka bima ya mikopo yao, kuongeza mapato ya Halmashauri na kutambulika kwa mifugo na umiliki wake.
Mradi mwingine uliotembelewa na mwenge wa uhuru uwekaji wa jiwe la msingi kituo cha afya cha Itiso ambapo awamu ya kwanza utagharimu kiasi cha shilingi milioni 250 ambazo ni fedha kutoka Serikali kuu mfuko wa fedha za tozo kwa jengo la wagonjwa wa nje ( OPD), jengo la maabara na kichomea taka.
Mradi utawezesha kusogeza huduma bora za afya karibu na jamii na kuimarisha afya ya jamii.
Mradi wa maji Dabalo pia ulikuwa miongoni mwa miradi iliyozinduliwa na mwenge wa uhuru ambapo utakuwa na uwezo wa kuhudumia jumla ya wakazi 8134 wa kijiji cha dabalo. Mradi utawezesha upatikanaji wa maji safi na salama kwa jamii, kumtua mama ndoo kichwani, kupunguza muda wa kutafuta majiau kuyafuata mbali na badala yake kufanya shughuli nyingine za maendeleo na kiuchumi. Pia kuondoa magonjwa ya mlipuko yanayosababishwa na kukosekana kwa maji safi na salama na udhibiti wa mapato yanayotokana na mradi wa maji baada ya kufunga mfumo wa mita za malipo ya kabla.
Mradi umegharimu kiasi cha shilingi 1,127,470,348.01,kwa mchanganuo fedha kutoka Serikali Kuu shilingi 1,033,617,241.13, wahisani(MKAJI) shilingi 91,663,906.88 na jamii shilingi 2,189,200.00.
Mwenge wa Uhuru pia ulizindua madarasa ya UVIKO 19 ßhuale ya sekondari Msangaambayo yamegharimu kiasi cha shilingi 60,000,000/=
Mradi wa kikundi cha vijana wasakatonge unaojishughulisha na utoaji wa huduma za ufundi seremala kwa wakazi wa kijiji cha Buigiri na vijiji jirani ambacho kilipewa mkopo wa shilingi 15,000,000/= na halmashauri ili waweze kupanua na kuboresha biashara yao.Fedha ambayo inatokana na asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri ambayo hutumika kuwezesha kundi la wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.0
Pia mwenge uliweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami Mvumi km 1.1 ambao utagharimu shilingi 496,928,000/= . Mkandarasi tayari ameshalipwa shilingi 348,794,730.00 kiasi cha shilingi 148,133,270.00 kitalipwa kwa kazi ya umaliziaji na fedha za matazamio. Mradi utawezsaha kuwa na barabara za kudumu na zenye kupitika muda wote.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.