Mkuu wa Mkoa wa Dodoma mheshimiwa Antony Mtaka ametoa ushauri kwa uongozi wa wilaya ya Chamwino kuwa na shule ya mfano wilayani hapo itakayabeba matokeo mazuri ya wilaya.
Mh Mtaka ameyasema hayo Januari 7, 2022 wilayani Chamwino alipokuwa na ziara ya kukabidhiwa vyumba vya madarasa katika kata za Chamwino, Msanga, Buigiri na Manchali wilayani humo.
'Kama wilaya mfikirie sasa kujenga shule moja ya ghorofa ambayo mtachukua wanafunzi bora toka kila kata watakaochaguliwa kusoma kwenye shule hiyo itakayowabeba kama wilaya kwenye matokeo ya kidato cha nne' amesema Mh Mtaka
Kwa upende wake Katibu tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi. Fatuma Mganga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa upendo kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma kwa ujumla kwa namna anavyouinua mkoa wa huo kwa kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu.
Pia ameziagiza shule za sekondari wilaya ya Chamwino kuwa na mpango mkakati wa wanafunzi kupata chakula cha mchana wawapo shuleni kwani kutainua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hao.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino Sr Donasiana Njuu amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwakutembelea Halmashauri ya Chamwino na kukubali kuzindua vyumba vya madarasa wilayani humo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.