Mkuu wa mkoa wa Dodoma leo tarehe 24.07.2021 amezindua Tamasha kubwa la nyimbo za cigogo lililofanyika katika kijiji cha chamwino Ikulu.. katika hotuba yake Mh Mkuu wa mkoa amemtaka muasisi wa Tamasha la nyimbo za Cigogo festival Dr Kedmon Mapana kulifanya tamasha hilo kuwa la kibiashara zaidi..
Akiongea katika ufunguzi huo Mh Mtaka amesisitiza kuwa Tamasha hilo lina fursa nyingi za kiuchumi zinazopatikana katika Tamasha hilo.
Ametaja baadhi ya fursa za tamasha hilo kwenye jamii ni kutoa elimu ya afya, kilimo na kujikinga na magonjwa mbalimbali kupitia sanaa na uimbaji.
wakati huo huo, Mkuu wa wilaya ya Chamwino Mh Gift Msuya ametumia nafasi hiyo kujitambulisha na pia kuwafahamisha wananchi wote kuwa ataanza ziara katika kata na vijiji vyote vya wilaya ya chamwino.
Tamasha hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo kamati ya usalama ya wilaya Makamo Mwenyekiti wa halmashauri, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya chamwino, Mh Diwani wa kata ya chamwino Ikulu na ma maafisa mbalimbali kutoka Wizara ya utamaduni , sanaa na michezo.
Mh Mkuu wa mkoa ameendelea kusisitiza kuwa kila mwananchi azidi kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19 Kwa kufuata maelekezo ya wataalam wa afya.
#ChamwinoKaziiendelee#
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.