Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule ameongeza muda wa siku mbili wa maonyesho ya wakulima 88 hadi Agosti10Mwaka huu ili kuongeza tija ya kilimo4 katika suala zima la kutoa Elimu kwa wakulima na
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameshauri kujengwa kwa Hosteli za wakulima katika Viwanja vya nanenane vilivyopo Nzuguni mkoani Dodoma ili wakulima wawe wanapata muda wakupata Elimu kuhusu kanuni za kilimo bora wakati ambapo maonyesho yatakuwa yameisha ili Kila Mwezi wakulima Kila Halmashauri waende kujifunza.
Hata hivyo ametoa Wito kwa Kila Halmashauri kupelekea idadi ya wakulima kufika katika maonyesho ya nanenane kupata maarifa na kujifunza masuala mapya yaliyopo katika sekta ya kilimo.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba amesema kuwa uzalishaji wa mazao agenda ya 10/30 mkoa umejipanga kuzalisha tani 600,000za Alizeti ili kuondokana na uhaba wa mafuta ya kula na kuongeza tija ya mazao.
Aidha Serukamba ameomba Maonyesho ya nanenane Kanda ya Kati yawe kwenye ramani ya Dunia ili kupanua wigo katika Nchi mbalimbali kushiriki ili Kampuni kubwa zenye teknolojia kutoa fursa ya kutoa Elimu kwa wananchi.
Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Mhina ametoa Wito kwa akulima na wafugaji kuhakikisha wanatumia Elimu walizopewa ili kuongeza uzalishaji wenye tija.
Pia amewataka wafugaji kutunza malisho na kutunza vyanzo vya Maji ili Mifugo iweze kupata Maji hata wakati wa kiangazi.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Pilly Mbaga ameuomba Uongozi wa Mkoa wa Dodoma kuyatumia Makampuni yanayojihusisha na kilimo kutoa Elimu kwa wakulima Kila Wilaya ili wajifunze na kutaka Makampuni hayo kushusha gaharama za Mbegu kutokana na wakulima wengi kushindwa kumudu gharama hizo.
Maonyesho hayo yameshirikisha wakulima mbalimbali toka katika Wilaya za Mikoa ya Singida na Dodoma.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.