Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule , amemshukuru Rais wa M
Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia , Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia shilingi takribani billion 12 za ujenzi wa bwawa la maji kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji, mradi unaotekelezwa katika kata ya membe iliyopo wilaya ya Chamwino.
Ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua mradi huo 01, februari 2023, amesema mradi huo ukikamilika utapunguza kilimo cha kutegemea mvua nakuanza kilimo cha umwagiliaji.
Mhe Rosemary alisema kilimo cha uhakika ni cha kisasa ili mazao yasikose maji baadaya mvua kukata.
“Mhe. Rais ameziweka kwasababu anajuwa kuwa wanachamwino wanahitaji kilimo mmekuwa ni wakulima wa siku nyingi na mmekuwa mkilima kilimo cha kutegemea mvua”.
“Uhakika wa kilimo cha kisasa ni cha umwagiliaji mvua inaisha unaendelea kumwagilia kwa hiyo mazao hayakosi maji hiyo ndio dhamira ya Mhe. Rais hataki tena kusikia Chamwino ina njaa,” Alisema Mkuu wa mkoa.
Hata hivyo amewataka wanachi kuhakikisha wanaulinda mradi huo na kukamilika kwa uhakika ili kutekeleza malengo yaliyokusudiwa kupitia mradi huo
Mkuu wa mkoa alisema fedha zinatolewa n Mhe. Rais kupitia Serikali kuu kwaajili ya utekelezaji wa miradi zifanyiwe kazi kwa wakati na kwa ubora ili wananchi waweze kupata huduma iliyokusudiwa.
Aidha amewataka wakandarasi kuwa makini katika utelekezaji wa miradi wanayopewa na Serikali, pia amewata mainjinia kuwepo eneo la mradi ili kuhakikisha utekuelezaji ukamilika kwa ubora unatakiwa.
“Lakini nisisitize sana leo tumepewa sisi wakandarasi wazawa wa kitanzania ni kwa upendo wa Mhe Rais kwa hiyo fanyeni kwa uhakika, mabwawa haya hayataki wizi yanataka umakini mkubwa bila kuruka hata hatua “.
“Wananchi kuweni walinzi wa kwanza katika huu mradi lakini dhamira ya Mhe. Rais wetu na Serikali fedha zikitolewa, miradi ifanyike kwa wakati na kwa ubora ili wananchi waende kupata huduma waliyoikusudia,” al
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.