Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Balozi Omar Mapuri ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Septemba 19, 2024 kushuhudia mafunzo yanayoendelea kwa siku ya pili ya uboreshaji wa daftari la kudumu la kupiga kura kwa maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata.
Mh. Balozi Mapuri ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Ndg. Tito P. Mganwa, afisa muandikishaji wa majimbo ya Chamwino na Mvumi Ndg. Godfrey Mnyamale pamoja na maafisa wa Tume hiyo kushudia mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi Mtendaji amemuhakikishia Mh. Balozi Mapuri kuwa Wilaya ya Chamwino itafanya vizuri katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la kupiga kura mwaka 2024 na kuvuka zaidi ya asilimia 72 ya zoezi lililopita.
Wakufunzi wa mafunzo hayo wameendelea kuwajengea uwezo maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata juu ya kutumia vifaa vya bayometriki (BVR) ili waweze kufanya zoezi hilo kwa umakini, kutunza vifaa hivyo na wao kwenda kutoa mafunzo kwa waendesha vifaa ngazi ya vituo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.