Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Staki Senyamule Februari 21, 2024 amefanya ziara ya kikazi Wilayani Chamwino ambapo amekagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Miradi iliyokaguliwa ni ya ujenzi wa shule ya mfano ya Mkoa ya wasichana, ujenzi wa uzio wa ofisi ya Halmashauri na zahanati ya kijiji cha Wilunze.
Akikagua miradi hiyo mkuu wa mkoa wa Dodoma ametoa maelekezo mbalimbali kwa wataalam na wasimamizi wa miradi hiyo ili ikamilishwe kwa haraka.
Wakizungumza kwenye ziara hiyo mhandisi wa Halmashauri anayesimamia mradi wa shule ya sekondari ya mkoa amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa majengo yaliyobaki yatakamilika ndani ya siku ishirini baada ya ziara ya Mkuu wa mkoa.
Aidha Mkuu wa Mkoa ameelekeza Zahanati ya Wilunze iwe imekamilika ifikapo tarehe 15 ya mwezi April, 2024.
Alipokuwa shule ya wasichana ya Mkoa wa Dodoma Mkuu wa mkoa alizungumza na wanafunzi wa kidato cha kwanza ambapo amewashauri kumrudishia shukrani Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa kusoma kwa bidii na kufaulu vizuri masomo yao.
Nao wanafunzi wamemshukuru Mhe. Rais kwa kuwajengea shule nzuri wametoa wito kwa wanafunzi wenzao ambao wamechaguliwa kuripoti shuleni mapema kwani masomo yamekwishaanza.
Vilevile Mkuu wa Mkoa amefanya mkutano wa hadhara ambapo amesikiliza na kujibu kero zilizotolewa na wananchi.
Ameutumia pia mkutano huo wa hadhara kuelezea mapokezi ya Fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo zilizopelekwa na Serikali kwenye kata hiyo, kuwa takribani zaidi ya shilingi bilioni tano (5) zimetekeleza miradi kwenye kata hiyo pekee, hivyo wanapaswa kumshukuru Mhe. Rais Mama Samia kwa kazi hiyo kubwa aliyoifanya kwenye kata yao.
Sambamba na ukaguzi wa miradi, Mhe. Senyamule amekagua eneo la uwanja yatakapofanyikia maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo kimkoa yatafanyika Wilayani Chamwino.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.