Mfuko wa dharula wa Rais wa Maerkani unaotekeleza mradi wa Mifumo ya sekta za Umma Awamu ya pili (Public Sector System Strengthing PS3) Kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wamefanya ziara ya pamoja katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kutathimini mahitaji ya kuboresha matumizi ya mifumo ya PlanRep na FFARS inayotumika kutoa huduma katika sekta mbalimbali zikiwemo Afya, Elimu na Kilimo.
Mradi huo wenye lengo la kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma kwenye Halmashauri za Wilaya unatarajiwa kutoa matokeo chanya kama vile kuwepo kwa mipango shirikishi iliyoandaliwa kwa kutumia takwimu zitokanazo na mifumo iliyoboreshwa, pia kushirikisha wananchi katika kuandaa mipango na bajeti na kusimamia utekelezaji wake, vilevile kuongeza ufanisi wa ukusanyaji na matumizi ya mapato ya Halmashauri.
Mratibu wa mpango huo Ndugu Otieno Godwin Osoro amesema kuwa kwa sasa mpango huu wa kutathimini mahitaji ya uwezeshwaji wa wadau kuboresha matumizi ya mifumo ya PlanRep na FFFARS upo katika hatua za mwanzo kabisa wa ukusanyaji takwimu ilikuweza kubaini mahitaji muhimu katika sekta mbalimbali kama vile Afya, Elimu na Kilimo ilikuwezakuboresha Mifumo hiyo.
Mradi huu unaowezeshwa na Mfuko wa Dharula wa Rais wa Marekani wa UKIMWI (USAID), Ulianza rasmi Julai 2020 na unatekelezwa katika Mikoa yote 26 Tanzania Bara na Zanzibar ngazi ya Taifa, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.