Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja amewaelekeza wahe. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kusimamia suala la wanafunzi kula chakula shuleni. Hayo ameyasema kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani wa mwaka uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Agosti 28,2024.
"Agenda ya chakula shuleni iwe ya kudumu kwenye mikutano yenu mnayofanya na wananchi, na tuwaelimishe wazazi na walezi chakula wanachokula shuleni ni kilekile ambacho mtoto angekula akiwa nyumbani." Alisema Mhe. Mayanja.
"Kuna wazazi wenginewanaona kama Chakula wanachokula shuleni ni kama anakula na watu wengine. Nadhani eneo hilo linahitaji elimu kwa sababu mtoto akila chakula shuleni inaweza kumuongezea ufaulu. Naomba tuwaelimishe wananchi." Alisema Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya pia ameongelea suala la changamoto ya uvamizi wa simba ndani ya Wilaya na na kwamba Serikali imeshachukua hatua ya kukabiliana nao.
"Tulipata changamotomya simba kwenye jata ya Ikowa, Msamalo, Manchali, Majeleko na sasa Chilonwa. Simba wale wamekuwa wakitoka kata moja kwenda kata nyingine. Kuna simba wawili wanaonekana wapo kwenye maeneo yetu. Serikali imeshachukua hatua, kikosi cha TAWA kiko hapa na TAWIRI wanafanya kazi ya kuhakikisha kwamba simba hawa wanaondoka katika maeneo yetu." Alisema Mkuu wa Wilaya.
Kwa upande wake Mhe. Edison Sweti Mwenyekiti wa Halmashauri ameeleza kuwa wameshakaa na wahe. Madiwani kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ya jinsi ya kujikinga na wakati huohuo askari wa wanyama pori wapo kwenye maeneo hayo ambayo simba wanaendelea kuzunguka, na tunashukuru simba hao tangu wameanza hawajamdhuru mwananchi yeyote ila tu wanadhuru mifugo ng'ombe na mbuzi.
Wakati huohuo mkutano mkuu umefanya uchaguzi wa Mkamu mwenyekiti wa Halmashauri ambapo kikanuni hufanyika kila baada ya kumaliza mwaka wa fedha na Mhe. Keneth Yindi amechaguliwa tena kuwa Makamu Mwenyekiti kwa mwaka huu wa fedha kwa kupata 100% ya kura za ndiyo ya kura zote zilizopigwa na wajumbe kutokana na kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.