Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesisitiza juu ya umuhimu wa sensa kwa makarani wa Sensa, wasimamizi wa maudhui na wasimamizi wa TEHAMA.
Ameyasema hayo alipotembelea kituo cha mafunzo ya usimamizi wa sensa Wilayani Chamwino leo Agosti 17, 2022 ambacho kipo shule ya sekondari Chamwino.
" Haya mnayoyategemea kuyafanya kilà mtu ndio anayaangalia. Mwisho wa mwaka mtu atakuwa anaomba takwimu. Naomba takwimu za mifugo ili nipange mipango, naomba niapte takwimu za wilaya za uchumi za uchumi wa wananchi wangu ili nipange mipango." Alisema mkuu wa mkoa.
Vilevile amesisitiza matumizi ya lugha kuwa lugha itakayotumika na makarani wa sensa iwe ni lugha fasaha na sahihi ya watanzania ambayo ni kiswahili. Hategemei watumie lugha ambayo wale wanàowauliza hawaielewi.pia amewataka watumie lugha yenye staha, lugha ambayo inaweza kueleweka lakini inatunza heshima ya unayeongea nae..
"Mtumie lugha yenye staha, lugha ambayo inaweza kueleweka lakini inatunza heshima ya yule ambaye unaongea naye. Lugha yenye staha ni lugha ambayoinamuonyesha mtu kuwa wewe ni rafiki yake, wewe ni ndugu yake, wewe ni Mtanzania mwenzake, lugha ambayo inamuondolea hofu ya kutokukuamini, lugha ambayo akikusikiliza atajenga imani kuwa ni mtu sahihi kwa sababu ni mtu anayeaminika." Alisema Mkuu wa mkoa.
Pia alizungumza kuhusu kujenga mahusiano mazuri na wale unaokwenda kuwahoji maswali, alitolea mafano unaingia kwenye kaya hujasalimia wenye nyumba unaanza moja kwa moja kuwahoji maswali. Kwa kufanya hivyo huwezi kupata taarifa za sensa kwani tayari utakuwa umempotezea shauku au hamu ya kukujibu.
"Sisi watanzania tunajua jinsi salamu ilivyo na umuhimu kwa utamaduni wetu." Alisema mkuu wa mkoa.
Aidha mkuu wa mkoa amesisitiza kuhusu suala la mavazi kuwa muonekano wa mavazi unaweza kumthibitishia unayemuhoji kuwa unaaminika na hivyo akajenga imani ya kukupa taarifa.
Alitilia mkazo suala la muda nakueleza kuwa waangalie mazingira wanayokwenda kufanyia zoezi la sensa, lakini kuwapangia muda watakaokwenda kuwahoji na kujipanga wao wenyewe. Ili kama ni nyumba ambayo huwa habaki mtu basi siku hiyo mtu awepo kwa ajili ya kutoa taarifa.
Aidha aliwataka watu wa TEHAMA kuitumia vizuri na kueleza kuwa TEHAMA imekuwa na mchango mkubwa sana kwa maendeleo lakini ikitumika vibaya imekuwa na madhara makubwa.
" Niendelee kusisitiza tumieni vizuri TEHAMA, ukikosea tu tarakimu moja mtu kakwambia anahekari 3 wewe ukaandika 33 hebu ona jinsi ambavyo umebadlilisha taarifa za matokeo ya tunachokitarajia na ambavyo utakwenda kuathiri mipango mnataka kuifanya. Kuweni makini na wale ambao wanajua hawako makini, zoezi hili wasilifanye. Maana hapo ndipo panakwenda kumalizia kazi nzuri ya kukusanya taarifa na kufanya mpate taarifa sahihi.' Alisema mkuu wa mkoa.
Makarani pia wametahadharishwa kumiepusha na ulevi mpaka watakapokuwa wamekabidhi kazi. Pia viongozi wengine wa kamati ya ulinzi na usalama walitoa tahadhari kwa mtu atakaye haribu zoezi la sensa kuwa atakuwa amefanya hujuma na hjvyo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Alitoa rai kwa wananchi wa mkoa wa dodoma kutoa taarifa sahihi bila hofu kwa makarani wa sensa kwa sababu wamewezeshwa na ana imani watafanya kazi nzuri kwani Serikari imejiridhisha nao. Aliomba wawaamini na wawape taarifa sahihi na zote ambazo zinatakiwa kutolewa.
Pia aliomba wannchi watoe taarifa pale ambapo watapata kikwazo kwenye zoezi la sensa. Na ili kutekeleza hilo alizindua namba maalum itakayotumika kupiga pindi inapotokea changamoto ambayo ni 0800110083.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.