Mafunzo kwa watendaji ngazi ya kata na waandishi wasaidizi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili yametolewa leo tarehe 14 Mei, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Business Center Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Ikumbukwe zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa awamu ya pili litaanza tarehe 16 Mei na kutamatika tarehe 22 Mei 2025 ambapo litahusisha mambo mbalimbali ikiwemo:
1 kuandikisha mpiga kura mpya mwenye umri wa miaka 18 na zaidi na atakayetimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi 2025.
2 kutoa kadi mpya kwa mpiga kura aliepoteza au kadi yake kuharibika
3 kutoa fursa kwa mpiga kura aliyoandikishwa kurekebisha taarifa zake ikiwemo majina na taarifa zingine
4 kuhamisha taarifa za mpiga kura aliyehama kutoka kata au jimbo alipoandikishwa awali
5 kuondoa taarifa za mpiga kura aliyepoteza sifa za kuwemo katika daftari kwa sababu mbalimbali ikiwemo kifo.
Hivyo, wataalam wa Halmashauri wakishirikiana na wataam kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wametoa mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo watakaohusika katika kuboresha taarifa katika daftari la kudumu la wapiga kura kutekeleza jukumu hilo kwa weledi
Aidha, zoezi hilo lilienda sambamba na kula kiapo cha utii, kutunza siri pamoja na kujivua uwanachama wa chama chochote cha siasa kwa watendaji hao.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Afisa Mwandikishaji wa Majimbo ya Chamwino na Mvumi Ndg. Godfrey Mnyamale ametoa wito kwa watendaji hao kwenda kutekeleza zoezi hilo kwa umakini na weledi ikiwa pamoja na kutumia lugha zenye stara kwa Wananchi na kuzingatia muda wa kufungua vituo vya uboreshaji wakati wote wa zoezi.
Vituo vyote vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.