Pichani ni watumishi wa Halmashauri ya Chamwino wakiwa kwenye mafunzo kuhusu mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji. Mafunzo hayo yametolewa na Tume ya Taifa ya Mipango ya matumizi bora ya Ardhi leo tarehe 10, Novemba Katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.Vijini vitakavyonufaika na mradi huu katika Wilaya ya Chamwino ni vijiji vinne vilivyopitiwa na mradi wa ujenzi wa Reli wa SGR. Katika mafunzo hayo imeelezwa kuwa sababu za kuwa na matumizi bora ya ardhi ni kudhibiti migogoro ya ardhi, kuondoa tatizo la baadhi ya watu kutokujua mipaka ya maeneo yao, maendeleo duni ya soko la ardhi,uharibifu waudongo na vyanzo vya maji, kudhibiti ufyekaji hovyo wa misitu, kudhibiti kasi ya kuhamahama na kudhibiti kuongezeka kwa ukame na jangwa
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.