Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amewataka Madiwani wa Halmashauri zote nchini kabla ya kupitisha bajeti za Halmashauri kuhakikisha wanakagua miradi ya maendeleo ili kujiridhisha na utekelezaji wa miradi hiyo.
Akiongea na Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda katika ukumbi wa Manispaa Waziri Ummy Mwalimu amesema madiwani wanao wajibu wa kusimamia na kutoa ushauri kwa Halmashauri katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Amesema kuwa usimamizi wa Halmashauri zote nchini uko chini ya mabaraza ya madiwani, lakini ipo changamoto ya wanaokwenda kukagua miradi ya maendeleo ni kamati ya fedha peke yake, hivyo kuanzia sasa kabla bajeti haijapatishwa madiwani wote wakakague miradi ya maendeleo.
“Haiwezekani madiwani wachache kwenda kukagua miradi ya maendeleo wakati bajeti ya Halmashauri inapitishwa na madiwani wote, je watajiridhishaje kuwa miradi hiyo imekamilika, hivyo naagiza kunzia sasa madiwani wote wakakague miradi ya maendeleo” amesisitiza Waziri Ummy
Amewataka madiwani hao kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalam katika kutekeleza Miradi ya maendeleo hasa sekretarieti ya Mikoa kwa kuwa ndio wenye wajibu wa kuzisimamia, kuzishauri na kutoa maelekezo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuweza kujenga na kuzistawisha Mamlaka hizo.
Aidha,amewataka madiwani wote nchini kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani na matumizi, pia kuhakikisha zikikusanywa zinapelekwa benki ndani ya masaa 24 na fedha hizo zitumike katika kutatua kero za wananchi
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.