Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Ally Gugu amewataka viongozi Wilayani Chamwino kutekeleza miradi kwa wakati na na kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa kwenye miradi hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa wakati wa ziara ya kukagua baadhi ya miradi inayotekelezwa katika Halmasahauri ya Wilaya ya Chamwino, tarehe Mei 05, 2023, na alipata nafasi kuzungumza na watumishi wa wilaya hiyo kwa lengo la kuweka mikakati bora ya utendaji kazi ili kufikia malengo ya maendeleo kwa uharaka.
“Tumebaini baadhi ya maeneo ambayo yamefanyika vizuri lakini yapo maeneo ambayo yanahitaji kuimarishwa. lakini angalizo kwenye maeneo yaliyobaki ya ujenzi basi tuzingatie yafanyike kwa umahiri zaidi lakini jengoi lizingatie viwango vya juu vya kupendeza.” Alisema Gugu.
Aidha Gugu ameipongeza Halmashauri kwa juhudi za utekelezaji wa miradi mbalimbali kupitia mapato ya ndani ikiwemo Zahanati ya Kijiji cha Wilunze ambapo ujenzi umefikia hatua ya umaliziaji.
“Kutokana na mapato ya ndani wenzetu wa Halmashauri waliweza kutenga fedha ambazo zimewezesha kuwa na jengo ambalo tayari tumejiridhisha liko kwenye hatua nzuri sana, na hivyo wahakikishe kazi inayoendelea isimamiwe ipasavyo hata umaliziaji wa jengo hili uweze kufanyika vizuri,”
Aidha Katibu Tawala Mkoa alieleza kuwa mradi huu wa zahanati ulikuwa katika miradi ambayo ya mwaka wa fedha 2021/2022 kwa hiyo tumeona upo nyuma na hivyo tulikubaliana tuhakikishe mradi huo unaanza kutoa huduma kabla ya mwaka huu wa fedha kuisha yaani tarehe 30, juni 2023.
Hata hivyo Gugu amesisitiza miradi inayotekelezwa kwa fedha za boost inapaswa kukamilishwa kwa wakati ifikapo juni 30, mwaka huu.
Katika ziara hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma alikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Zahanati ya Kijiji cha Wilunze ambavyo ujenzi wake unaendele na Mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya maabara ya baiolojioa na kemia katika shule ya sekondari msanga ambapo mradi upo hatua ya umaliziaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.