DAS AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 63 YA UHURU
Kuelekea maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Tanzania Bara, Katibu Tawala (DAS) wa Wilaya ya Chamwino Bi. Neema Nyalege amemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mh. Janeth Mayanja kuongoza zoezi la upandaji miti katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino lillilofanyika katika shule ya Chamwino Sekondari.
Zoezi hilo limeshirikisha pia watu mbalimbali wakiwemo watumishi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Chamwino, Meneja wa Wakala wa Misitu (TFS) Wilaya ya Chamwino Ndg. Samwel Matula na Wananchi mbalimbali ambao kwa pamoja walishiriki zoezi la upandaji miti.
Zoezi hilo pia limejumuisha upandaji wa miti ya matunda na kivuli na baadhi ya miti iliyopandwa ni miti aina ya Mipera pamoja na Miashoki
Wananchi mbalimbali pia waliendelea na zoezi la upandaji miti wa zaidi ya miche 25,000 iliyotolewa na Wakala wa Misitu (TFS) Wilaya ya Chamwino katika maeneo yao ya makazi na biashara ikiwa ni moja ya njia ya kuenzi miaka 63 ya uhuru wa Tanzania Bara.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.