Na Brian Machange
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino yatoa elimu ya kupinga vitendo vya vya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa shule ya msingi Izava na kwa wazazi wa eneo hilo hivi karibuni katika kampeni ya siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia.
Mratibu wa Mradi wa Mwanamke Jasiri (CCT) Mkoa wa Dodoma, Bi. Elizabeth Ngede ametoa ufafanuzi kwa wanafunzi na wazazi wa eneo hilo kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia havikubaliki hivyo vipigwe vita katika ngazi zote kuanzia kwenye familia.
Naye Mratibu wa Dawati la maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Chamwino Bi. Sophia Swai amekemea vikali dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimekuwa vikiikumba jamii hasa katika Kata ya Segala.
Bi. Swai amebainisha baadhi ya vitendo vya ukatili vinavyoikumba Kata ya Segala nipamoja na kutokusomesha watoto wa kike elimu ya juu, kuwaozesha watoto wadogo, kuwanyima watoto majina halali ya baba zao pindi wanawake wanapotelekezwa , kuthamini mgeni anapokutembelea zaidi ya watoto ya watoto wako. Kwa kufanya hivi haya yote yanawanyima haki watoto katika familia.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.